Pepsi wamelazimika kuomba radhi juu ya tangazo lao la makosa nchini Sweden wakimuonyesha Cristiano Ronaldo katika kikatuni kilichokuwa na mfano wa Cristiano Ronaldo.
Kitangazo hicho kilionyeshwa siku ya mchezo wa mkondo wa pili kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia (World Cup play-off) baina ya Ureno na Sweden, mchezo ambao Ronaldo alipiga 'incredible hat-trick' na kuipeleka Ureno Brazil.
Ronaldo alifananishwa na mdoli ambao ulilazwa katika njia ya treni na baadaye kupigwa picha iliyokuwa na maneno chini yake yaani 'caption' iliyosomeka
'We're going to pass over Portugal.'
Tangazo hilo limezua mtafaruku huko katika klabu ya Real Madrid ambako kundi moja la mtandao wa kijamii wa Facebook la klabu hiyo liliandika kwa maneno yaliyosomeka
'I'll never drink Pepsi' na kupendwa na watu 115,000 (yaani watu walio like hiyo komenti).
Wanachama wa kundi hilo katika mtandao wa kijamii wamesema hiyo ni aina nyingine kutangaza kinywaji hicho mjini Stockholm.
'We
regret if people were offended by the posts; they were immediately
taken down. We would like to extend our apologies to all concerned.'
Pepsi ni wadhamini wakubwa mpinzani wa Ronaldo amshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
No comments:
Post a Comment