Winga wa Bayern Munich Franck Ribery ameondolewa kikosini kuelekea katika mchezo mkubwa wa Jumamosi wa ligi kuu ya soka nchini nchini Ujerumani dhidi ya Borussia Dortmund
kufuatia kuvunjika mbavu.
Mfaransa huyo pia ataukosa mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow wiki ijayo.
Ribery
amepatwa na maumivu hayo wakati akifanya tackling nyingi katika mchezo baina ya Ufaransa dhidi ya Ukraine ambao Ufaransa ilishinda mabao 3-0 Jumanne na kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza kombe la dunia mwakani.
Msemaji wa Bayern Markus Hoerwick amenukuliwa kupitia mtandao wa kijamii wa twitter akisema
'Tutamkosa Ribery dhidi ya Dortmund,'
'Franck ametonesha mbavu zake katika mchezo wa kimataifa.
Kuna wasiwasi kwenye mchezo Jumatano mjini Moscow'
Bayern, ambayo haijapoteza katika michezo 37 ya ligi inaongoza msimamo wa ligi ya Ujerumani Bundesliga wakiwa na alama 32 points, alama nne mbele ya wanawafuatia Dortmund.
Kuelekea katika mchezo huo Dortmund
nayo kwa upande wao wanamajeruhi kadhaa kutoka kikosi cha kwanza wakiwemo walinzi wa kati Mats Hummels na Neven Subotic pamoja na kiungo Ilkay Gundogan.
No comments:
Post a Comment