KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 12, 2012

RONALDO DE LIMA:BRAZIL IKO KATIKA PRESSURE KUBWA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA 2014, LAKINI PIA NEYMAR NI BORA ZAIDI YA MESSI. MOURINHO ANASEMA TUZO YA BALLON D' OR ANASTAHILI KUPEWA CRISTIANO RONALDO.


Ronaldo: Brazil itakuwa katika shinikizo kubwa la kufanya vizuri kombe la dunia 2014
Mshambuliaji nyota wa zamani wa kimataifa wa Brazil Ronaldo de Lima, anadhani kuwa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitakuwa katika shinikizo kubwa la kutakiwa kufanya vizuri wakati taifa hilo litakapo kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia 2014, lakini anaamini kuwa hiyo itawajengea zaidi morali wachezaji wa timu hiyo.

Ronaldo De Lima mwenye umri wa miaka 36 alistaafu kucheza soka mwaka 2011 baada ya kufunga jumla ya magoli 62 goals baada ya kuitumikia timu ya taifa ya Brazil ‘Selecao’ jumla ya michezo 98 lakini pia akivitumikia vilabu vikubwa duniani vikiwemo Barcelona, Real Madrid na Inter Milan. 

Amesema kutakuwa na mengi yatakayokuwa yakitegemewa kwa wenyeji hao katika kipindi hiki cha miaka miwili kuelekea katika fainali hiyo, huku kocha wa Brazil Mano Menezes akiendelea kukijenga kikosi lakini anaamini kueleka kwenye michuano hiyo Brazil itaibua wachezaji bora.

Amenukuliwa De Lima akisema,
"najua itakuwa ngumu kwa kikosi cha Brazil hususani katika kipindi hiki cha kuimarisha timu"
"hakuna shaka kuwa kucheza nyumbani kutaleta ‘pressure’ , lakini hii itakuwa ni namna ya kujenga upya ari ya kikosi"

Katika hatua nyingine Ronaldo amesema, mshambuliaji Neymar anaweza kuwa mchezaji mzuri zaidi ya Messi endapo ataelekea kucheza solka barani Ulaya.

Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Barcelona na Real Madrid amesisitiza kuwa wakati mu-Argentina Messi akiendelea kung’ara  duniani kwasasa, anaamini mshambuliaji Santos Neymar ana uwezo wa kumzidi Messi.

Mourinho: Itakuwa kosa kubwa kama Ronaldo hata shinda tuzo ya Ballon d'Or
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anadhani kuwa Cristiano Ronaldo anastahili kushinda tuzo ya Ballon d'Or na kusema kuwa mshambuliaji huyo yuko katika kiwango kingine ukilinganisha na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.

Mourinho amesema baada ya mchezo mkubwa wa Clasico, wachezaji wote hao walikuwa katika sayari nyingine lakini sasa amepata wazo jipya kuhusu kauli yake hiyo ya awali, ambapo  anaamini mshambuliaji wake Cristian Ronaldo ni bora kuliko mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi.

Amenukuliwa akisema,
"itakuwa ni kosa la jinai endapo Cristiano hatashinda Ballon d'Or. 

Kama Messi ni bora duniani ni kwasababu Cristiano anatokea katika sayari nyingine" 

"Hajazaliwa Madeira, lakini katika sayari ya Mars. Kwa hiyo hatokei katika sayari ya dunia. Ndio maana ni mchezaji bora ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment