KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 12, 2012

Benzema: Nataka kuwa mwenye mafanikio kama Zidane


Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema amesema angependelea kuona anapata mafaniko makubwa kama Zinedine Zidane.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliyejiunga na Madrid akitokea Olympique Lyonnais katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2009, anatarajia kupata mafanikio kama ilivyokuwa kwa Zidane, na mara kadhaa amekuwa akimuomba ushauri nguli huyo.

Amenukuliwa Benzema akisema,
"nilikuwa nikimpenda Zidane sana kwasababu na ilikuwa ndoto yangu. 

Nimekutana naye na kuongea naye. Nilikuwa nafuraha sana.
"nimekuwa mara zote nikimuomba ushauri na alikuwa akinipa. Nategemea nitakuwa mtu tofauti na yeye, lakini mwenye mafanikio kama yeye."

Benzema pia ametumia fursa hiyo kumpongeza na kumsifia mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo De Lima ambaye alikuwa ndiye mtu wa mfano ‘Idol’.

"ulikuwa ni msimu wangu wa kwanza katika klabu hii ya Madrid, na nilipata fursa ya kukutana na Ronaldo,"
"nilimfuata kama mtoto na nilivutiwa naye. 
Kwangu mimi ni mchezaji mkubwa wa kipindi chote"