KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 9, 2012

KAGERE NA NIYONZIMA KUONGOZA YANGA DHIDI YA JKT RUVU KESHO TAIFA

Meddie Kagere mshambuliaji mpya Yanga
Mtihani wa kwanza wa kocha mpya wa Yanga Thom Saintfiet akiwa kama incharge wa benchi la ufundi ni hapo kesho atakapo kuwa akiiingoza Yanga kama kocha katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu mchezo wa kirafiki utakao pigwa katika uwanja wa taifa hapa jijini Dar es Sa laam .
Yanga ambayo imefanya usajili ambao umewapendeza mashabiki wake itakuwa ikionyesha soka yake kwa mara ya pili baada ya usajili kuanza lakini mara hii ikiwa chini ya Mbelgiji Saintfiet kwa mara ya kwanza.
Mbelgiji huyo ambaye anasafari ya kuifundisha yanga miaka miwili ya mkataba wake amekuwa akifurahia kikosi chache kilicho sajiliwa na kamati ya Usajili chini ya Salum Rupia akisaidiana na Seif Ahmed na Abadalah Bin Kleb bila shaka kitaonyesha kandanda ya matumaini kwa mashabiki wake katika uwanja wa Taifa hiyo .
akizungumzia mchezo wa kesho afisa habari wa yanga Luis amesema wanatarajia kuonyesha wachezaji wengine wawili ambao bado kuonekana ambao wameorodheshwa katika orodha ya wachezaji wapya akiwemo Meddie kagere.
Niyonzima kiungo wa Yanga
katika mchezo dhidi ya mabingwa wa soka wa Uganda Express mchezo ambao Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-1 , yanga ilimkosa kiungo wake hodari Haruna Niyonzima hivyo basi huenda raha ya mchezo wa kesho ikachagizwa na kiungo huyo kwa upande mwingine.

No comments:

Post a Comment