KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 28, 2012

KOMBE LA KAGAME:YANGA BINGWA MARA MBILI KOMBE LA KAGAME.

Hatimaye Yanga imefanikiwa kutetea taji lake la michuano ya kombe la Kagame baada ya kuifunga timu ngeni kwenye mashindano hayo Azam, kwa  mabao 2-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda Hamis Kiiza alifunga bao la kwanza dakika ya 44 na Said Bahanuzi akaongeza bao la pili ndani ya dakika za nyongeza.
Yanga wamezawadiwa dola 30,000, Azam wao wamepata dola 20,000 na Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo walioifunga APR ya Rwanda 2-1 kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu, wameondoka na dola 10,000.
Fedha hizo zimetolewa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye ni mdhamini wa michuano hiyo kwa miaka zaidi ya 10 na mashindano hayo yamepewa jina lake.

No comments:

Post a Comment