Mohamed Aboutrika amesaidia Misri kupata ushindi wa
mabao 4-2 dhidi ya Guinea katika michuano ya kufuzu kushiriki kombe la
dunia kwa timu za Afrika. Hii ni mara ya miamoja kwa Aboutrika kuchezea
Misri.
Misri sasa imekuwa timu ambayo haijashindwa katika michuano hii ya kufuzu kwa kombe la dunia litakalochezwa Brazil mwaka ujao.
Tayari Misri ilikuwa imeshinda kundi G na kufika fainali ya michuano ya kufuzu kwenda Brazil.
Lakini Guinea, ambayo ni ya pili kwenye kundi
hilo, iliweza kujipatia bao moja ambalo mchezazi wa Misri Adam El-Abd
aliingiza kwenye lango lao.
Na ilichukua muda kwa Misri kurejea katika hali ya mchezo mzuri na kisha kuingiza bao lengine mnamo dakika ya 38.
Dakika nyengine nne baada ya kipindi cha
mapumziko, mchezaji Kamil Zayatte, aliondoshwa uwanjani na Misri kutumia
fursa hiyo huku Aboutrika akiingiza bao lengine ambalo liliiweka Misri
mbele
Guinea haikufainikiwa kujikwamua pakubwa baada
ya kujiongeza bao lengine moja tu kupitia kwa mchezaji Seydouba Soumah
wakiwa wamesalia wachezaji 10 baada ya mwenzao konyeshwa kadi nyekundu
Mohamed Salah aliingza bao la tatu kwa Misri na
baadaye mnao dakika ya 83 Guinea mchezaji wa Guinea akapiga shuti kwenye
lango lao wenyewe na kuipa Misri ushindi wa mabao manne kwa mawili.
Matokeo hayo yaliipa Misri hadhi ya kuwa timu ya pekee kushinda katika makundi kwa kuwa na pointi 18.
No comments:
Post a Comment