Wachezaji wa Tanzania wa Olympic |
Jumla ya wanamichezo
sita wa Tanzania waliofuzu vigezo vya kushiriki michezo ya mwaka huu ya Olympic
wameagwa rasmi hapo jana katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa HYYAT
REGENCE zamani Kempisk katikati ya jijini la Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali
wa vyama vya michezo walihudhuria HAFLA hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mgeni
rasmi naibu waziri wa habari michezo na utamaduni Amos Makala, viongozi
mbalimbali wa kamati ya Olympic Tanzania na wanamichezo wenyewe ambao
wanatarajiwa kuondoka nchini hapo kesho kuelekea jijini London kushiriki
michezo hiyo
Waziri
makala katika hotuba yake amewataka wanamichezo hao kujiamini na kujituma huku
wakijua kuwa mamilioni ya watanzania wako nyuma yao na wanasuburi medali zao kwa
hamu kubwa.
Amesema
anaamini wamepata maandalizi ya kutosha chini ya kamati ya Olympic.
Lakini pia
waziri makala alitumia fursa hiyo kuwataka wadau wajitokeze kudhamini na
kufadhili michezo nchini huku akiwapongeza kampuni ya coca kola ambayo
imedhamini safari kwa wanamichezo hao ambao kesho watakuwa wakiandamana na
vikongozi wao.
Wakati TOC
ikisema itatoa shilingi milioni kumi kwa
atakaye fanya vizuri huku waziri wa zamani wa michezo wa zamani Mrisho Sarakikya
katika kujaribu kuwapa hamasa zaidi amesema yuko tayari kutoa dola elfu mbili
kwa yeyeto aatakayerudi nyumbani na medali.
Wachezaji watakao
ondoka kesho ni pamoja na Msenduki Mohamed,Samsoni Ramadhani ambaye atakuwa
nahodha,Mgdalena Mushi, selemani Kidunda Zakaria Mrisho na Faustine Musa.
No comments:
Post a Comment