Mabingwa
watetezi wa michuano ya Copa Coca-Cola, Kigoma wameng’oka katika
michuano ya mwaka huu baada ya kulala mabao 2-1 mbele ya Mara katika
mchezo uliochezwa leo (Julai 7 mwaka huu) Uwanja wa Tanganyika Packers
ulioko Kawe, Dar es Salaam.
Hadi
kipindi cha kwanza cha mechi hiyo ya kutafuta tiketi ya kucheza robo
fainali kinamalizika, Mara walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa
dakika ya 21 na George Martime.
Kipindi
cha pili kilianza kwa nguvu ambapo Mara walifanikiwa kupachika bao la
pili dakika ya 52 kupitia kwa Israel Daud. Kigoma ilipata bao lake
dakika ya 63 mfungaji akiwa Hassan Ramadhan.
Kwa
ushindi huo sasa Mara itacheza mechi ya robo fainali Julai 10 mwaka huu
saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Karume na mshindi wa mechi kati ya
Morogoro na Pwani itakayochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Tanganyika
Packers.
Nayo
Temeke imepata tiketi ya kucheza robo fainali baada ya leo kuitoa
Ruvuma kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya 16 bora iliyofanyika
Uwanja wa Karume. Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo
zilikuwa zimefungana mabao 2-2.
Katika
mikwaju ya penalti, Temeke ambayo itcheza robo fainali Julai 10 mwaka
huu saa 2 asubuhi kwenye Uwanja wa Karume na mshindi wa mechi kati ya
Mjini Magharibi na Kagera inayochezwa leo jioni kwenye uwanja huo
ilipata penalti 3 dhidi ya moja ya wapinzani wao.
No comments:
Post a Comment