KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 7, 2012

KAGAME CUP:S VITA YA DR CONGO, URA YA UGANDAKUTUA DAR JULAI 12


Vita club ya DR Congo
URA ya Uganda
Timu za AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na URA ya Uganda zinatarajia kuwasili nchini Julai 12 mwaka huu kushiriki michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 14 mwaka huu. 
 
AS Vita Club ambayo iko kundi A pamoja na timu za Simba (Tanzania Bara), Ports (Djibouti) na URA itawasili saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikipitia Nairobi.  Nayo URA itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jioni ya siku hiyo kwa ndege ya Air Uganda. AS Vita imepangiwa kufikia hoteli ya Rombo Green View wakati URA itakuwa hoteli ya Royal Valentino.

No comments:

Post a Comment