Serena Williams kutoka Marekani amemshinda
Agnieszka Radwanska wa Poland 6-1 5-7 6-2 kujishindia taji la wanawake la
mashindano ya kila mwaka ya Wimbledon.
Hii ni mara
ya tano kwa Serena kushinda mashindano haya, ikiwa ni mara yake ya 14 kushinda
mashindano ya kiwango kikubwa kama hiki(Grand slam).
Serena
alianza vizuri kwa kitisho seti ya kwanza akionyesha dalila za kumaliza kazi
kwa haraka alipomchapa Radwanska 6-1 seti ya kwanza iliyomalizika kwa mda mfupi
kuliko ilivyotarajiwa.
Hata hivyo
mambo yalibadilika katika seti ya pili wachezaji hawa waliporejea baada ya
kukwepa mvua iliyosababisha mechi kusimama kwa mda wa dakika 25 .
Radwanska
alianza kuonyesha dalili za kurejea na kujiamini kuweza kunyakua ushindi kutoka
kwa mkongwe wa mashindano haya na kuondoka na ushindi wa seti ya pili 7-5.
Seti ya tatu
ilipoanza, Serena lionyesha ukomavu wake na uzowefu kwa kumdhibiti mpinzani na
kutumia kila mbinu alizo nazo akiweka rekodi ya ''ace'' kupiga mashuti ya mpira
bila kuguswa, na sasa ametimiza 'ace' 100 akimpita Philipp Kohlschreiber wa
Ujerumani ambaye anashikilia rekodi ya ace 98.
Kabla ya
pambano la leo Serena alikua na jumla ya 'ace' 85, kwa hiyo katika mechi ya leo
ametumia ace'15 kuweza kumpiku raia wa Poland.
Hivyo ndivyo
Serena alivyoweza kuuchangamsha uwanja wa Wimbledon na kunyanyua ngao ya
'rosewater dish' inayowaniwa na wanawake kwenye uwanja wa Wimbledon kila mwaka.
No comments:
Post a Comment