Kiungo wa Manchester
United Ryan Giggs ametangazwa kuwa nahodha wa kikosi cha kocha Stuart Pearce
kuongoza Great Brotain kwenye michezo ya Olympic.
Raia huyu wa
Wales ni miongoni mwa wachezaji watatu wenye umri mkubwa zaidi ya miaka 23
ambao wanaruhusiwa kushiriki michezo hiyo akiungana wa waingereza wengine Craig
Bellamy na Micah Richards kwenye Olympic London 2012.
Giggs ameshinda
jumla ya mataji 12 ya Premier League,mataji manne ya FA na mataji mawili ya Champions
Leagues ndani ya kipindi chake cha miaka 21 ya kucheza soka Old Trafford.
Giggs mwenye
umri wa miaka 38 kwasasa amesema "ni
wazi nina uzoefu . kama nahodha nina matumaini ninaweza kuambukiza uzoefu wangu
wachezaji vijana."
GB itacheza
dhidi ya Brazil mchezo wa kirafiki July 20 katika uwanja wa 20 Middlesbrough wa
Riverside Stadium.
Imepangwa katika
kundi la A na nchi za Senegal, Uruguay na United Arab Emirates na itakuwa
ikicheza michezo yake katika viwanja vya Old Trafford, Wembley na Millennium
Stadium.
No comments:
Post a Comment