Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mjumbe wake wa
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani
Semlangwa kilichotokea Julai 5 mwaka huu kutokana na maradhi.
ACP Semlangwa ambaye alizikwa
juzi (Julai 6 mwaka huu) katika Kijiji cha Gumba, Wilaya ya Kisarawe mkoani
Pwani alitoa mchango mkubwa akiwa mjumbe wa Kamati hiyo inayoongozwa na Kamishna
wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana.
Msiba huo ni pigo kwa familia
ya ACP Semlangwa, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na
mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho akiwa mjumbe wa kamati hiyo.
TFF inatoa pole kwa familia
ya marehemu ACP Semlangwa, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu
katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa
familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke roho ya marehemu
ACP Shabani Semlangwa mahali pema peponi. Amina
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment