KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 16, 2012

AFC LEOPARDS YAMUACHA VICTOR OCHIENG ZIARA YA TANZANIA.KUCHEZA NA SIMBA JUMAPILI.


 

Victor Ochieng, ambaye ni majeruhi ameachwa katika kikosi cha AFC Leopards ambacho kinakuja nchini kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara ‘Vodacom Tanzanian Premier League’ Simba SC na mchezo mwingine dhidi ya mabingwa wa kombe la Kagame Yanga FC.
Walinda mlango Patrick Matasi na Barnabas Tiema ni miongoni mwa wachezaji walioko katika ziara hiyo na watakuwa wakiambatana na walinzi Martin Imbalambala, Eric Masika, Idrissa Rajab, Jonas Nahimana, Abbass Kiwalabye na Amon Muchiri.
Viungo ni Bernard Mangoli, Laurent Tumba, Edwin Wafula, Paul Were, Charles Okwemba na Floribert Tambwe.
washambiliaji katika kikosi cha kocha Jan Koops ni Jimmy Bageya, Allan Wanga, Oscar Kadenge na Mike Barasa.
Kikosi hicho kitakuwa safarini hapo kesho kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza utakaopigwa jumapili dhidi ya Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abed Kaluta .
Baada ya mchezo huo Leopards wataelekea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa pili dhidi ya Yanga uliopangwa kuchezwa  August 22.
Kikosi kamili
Goalkeepers: Patrick Matasi, Barnabas Tiema.
Defenders: Martin Imbalambala, Eric Masika, Idrissa Rajab, Jonas Nahimana, Abbassi Kiwaalabye and Amon Muchiri.
Midfielders: Bernard Mangoli, Laurent Tumba,Edwin Wafula, Paul Were, Charles Okwemba and Floribert Tambwe.
Strikers: Jimmy Bageya, Allan Wanga, Oscar Kadenge and Mike Barasa.

No comments:

Post a Comment