KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 20, 2012

BAADA YA KUICHAPA AFRIKAN LYON, YANGA YAELEKEA RWANDA.




 
 

Kikosi kamili cha mabingwa wa kombe la Kagame Yanga ya Dar es Salaam kinaondoka nchini hii leo kuelekea nchini Rwanda ambako kitakuwa kikiendelea na program yake ya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu ya kandanda Tanzania bara.
Ikiwa nchini Rwanda, Yanga chini ya kocha Thom Seintfiet itacheza michezo kadhaa ya kirafiki nchini humo kabla ya kurejea nchini kuendelea na maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom ambayo bado haijathibitishwa itaanza rasmi lini.
Jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrikan Lyon na kupata ushindi wa mabao 4-0 huku mabao ya Yanga yakiwekwa kwenye kamba na kiungo Harona Niyonzima aliyefunga mabao mawili
,Simon Msuva na Jerison Tegete (Tazama matukio katika picha).
Akiongea na Rockersports katibu wa Yanga John Selestine Mwesigwa amesema kikosi hicho cha Yanga kitakuwa huko kwa wiki moja na kitarejea nchini tarehe 27/08/2012 tayari kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa ligi.
Amesema mlinzi mpya katika kikosi hicho ambaye amejiunga na Yanga msimu akitokea mabingwa wa soka nchini Rwanda APR Mbuyi Twite ataungana na wenzake wakati wakiwa nchini  Rwanda.

BOFYA HAPA KUSIKILIZA

No comments:

Post a Comment