Roberto
Mancini ana matumaini kuwa Manchester City itakamilisha usajili wa wachezaji
watani wenye thamani ya pauni milioni £40 kabla ya muda wa mwisho wa usajili
kufungwa usiku wa leo.
Mancini
anamfukuzia mlinzi wa kulia wa Inter Milan Maicon, mlinzi wa kati wa Fiorentina
Matija Nastajic na kiungo wa Benfica Javi Garcia. Lakini pia anategemea
kuwasajili Richard Wright na Scott Sinclair kuthibitishwa kama wachezaji wa City
kwanza.
Sinclair
amethaminishwa kwa pauni milioni £6.2, Maicon £4 na Garcia zaidi ya pauni milioni
£20 wakati Nastajic amethaminishwa kwa pauni milioni £11 lakini City haitalipa
pesa kamili kwasababu Stefan Savic anaelekea Italia kwa mpango wa kubadilishana.
Baada
ya kuwa katika kipindi cha kuchekecha cha kiangazi City imefanikiwa kumsajili Jack
Rodwell pekee ambapo kwasasa wanakamilisha biashara katika siku ya mwisho.
Amenukuliwa
Mancini akisema
"endapo
tutakamilisha mipango hii tutaimarisha timu yetu. Tunazungumza kuhusu mchezaji
mmoja mkubwa unapomtaja Maicon, kwasababu anauzoefu na kijana Nastajic atakuwa
mlinzi mzuri kwa muda mrefu."
Meneja
huyo wa City anadhani Sinclair kama ni mbadala wa Adam Johnson aliyeuzwa lakini
amesisitiza kuwa winga huyo wa Swansea hana uwezo wa kukokota mpira kama
mchezaji mpya wa kutoka Sunderland.
"Sinclair
anacheza nafasi moja kama Adam lakini tofauti ni kuwa Adam anatembea na mpira
mguuni na Sinclair anatembea saba akiwa kwenye nafasi ".
City
kesho itakuwa na kibarua dhidi ya QPR bila ya majeruhi kadhaa Gareth Barry,
Micah Richards na Sergio Aguero.
Allegri aambiwa
kavukavu
Massimiliano
Allegri ameambiwa waziwazi kuwa yeye na vijana wake wanapaswa kupigania taji la
Serie A kwa udi na uvumba hasa baada ya kuwasili kwa Nigel De Jong.
Kampeni
ya msimu huu imeanza wakati ambapo Rossoneri ikiwapoteza wachezaji wake muhimu
kama Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva. Wengine ni Alessandro Nesta, Clarence
Seedorf na Pippo Inzaghi.
Baada
ya kufungwa na Sampdoria, kumekuwepo na hali ya sintofahamu kiasi majaliwa ya
hatma ya Allegri kumaliza msimu kuwa mashakani hasa ukifuatilia mahojiano ya Adriano
Galliani aliyofanyiwa na La Gazzetta dello Sport.
Amenukuliwa
makamu wa Rais wa Milan na Sports Daily akisema
"kwasasa
Allegri hana sababu tena hapa Milan, shukrani kwa usajili wetu wa wachezaji
wanne ambapo tutakuwa tunarejea katika mbio za kusaka Scudetto.
“De
Jong ni mmoja wa wachezaji wazuri na nguvu ulaya kwasasa anajua kazi na atatufanyia
kazi”.
"tofauti
kati yetu na wapinzani wetu sasa imepunguzwa Allegri hatakiwi kuficha hilo. Tunataka
kucheza na kushinda taji si kumaliza katika nafasi ya tatu"
No comments:
Post a Comment