KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 1, 2012

WAAMUZI WA SOKA WAPIGWA MSASA KWENYE SEMINA. ZINGATIENI KUTENDA HAKI .

Mkufunzi Leslie Liunda akifundisha waamuzi wa daraja la kwanza waliohudhuria semina ya ufunguzi wa VPL msimu 2012/2013 kwenye ukumbi uliopo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Picha na Rahel Pallangyo.

Waamuzi wakimsikiliza Sunday Kayuni kwenye semina ya maandalizi ya kuanza kwa ligi kuu ya soka Bara.
Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Sunday Kayuni akitoa neno kwa waamuzi kabla ya kuanza ligi kuu Tanzania Bara

Waamuzi wa kike wakiwa katika mtihani wa kukimbia ikiwa ni sehemu ya semina ya waamuzi.
MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni amewaasa waamuzi kutumia filimbi yao vizuri ili kutenda haki wanapo kuwa uwanjani.

Kayuni aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa  semina ya waamuzi wa daraja la kwanza kituo Dar es salaam inayofanyika Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2012/13.

Amesema waamuzi ni kiungo muhimu  katika kuendeleza mpira nchini, endapo watakuwa mahakimu wazuri wakiwa uwanjani.

Amewataka waamuzi hao  kuchezesha kwa kufuata sheria 17 za soka, ili waweze kusaidia soka la Tanzania kusonga mbele.

Kayuni amewatahadharisha kuwa wanapochezesha vibaya wanajiharibia wao wenyewe, kwani mchezo wa soka una mashabiki wengine na unaonyeshwa karibu kila sehemu kutokana na teknolojia kukua.

"Endapo mtarubuniwa na viongozi wa vyama vya soka FA wanapokwenda kuchezesha mtoe taarifa kwa maandishi katika  ofisi yangu itawashughulikie kulikoni waamuzi kuendelea kuumia au kuwa mbuzi wa kafara," alisema Kayuni.

Hata hivyo, alisema amekuwa akisikia malalamiko kwa pembeni, lakini hajafikishiwa kwake.
Alisema amepata taarifa kuwa wanapokwenda mikoani kuchezesha viongozi wa FA wanawashinikiza timu zao zishinde na mnapoacha kutekeleza matakwa yao wanawanyima posho zao.

Jumla ya waamuzi wapatao 190 kutoka mikoa yote wameudhuria semina na kufanya mtihani ya utimamu  wa mwili. Semina hii inaratajiwa kufungwa kesho jioni.

No comments:

Post a Comment