KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 16, 2012

KIMENUKA USAJILI WA YONDANI NA LIDONDO, MGONGOLWA UKO WAPI?.

Mwenyekiti wa kamati ya katiba ,sheria na hadhi ya wachezaji tff.



Kuelekea kuanza kwa msimu mpya ligi kuu ya soka Tanzania 2012/2013, vilabu vyote shiriki vimewasilisha majina ya wachezaji wao ambapo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina hayo ilikuwa ni saa 11 jioni ya jana huo ukiwa ni baada ya kuongezwa siku tano mbele.
Katika kuwasilisha majina hayo klabu ya mwisho ilikuwa ni wana Kishamapanda Toto Afrika ya Mwanza ambao walikamisha idadi kamili ya vilabu vyote kumi na nne.
Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Angetile Oseah amesema pamoja na zoezi hilo kukamilika kwa wakati kama ilivyo tangazwa lakini bado kuna matatizo kadhaa ambayo ofisi yake imeyaona ambayo kimsingi yatapelekwa katika kamati katiba sheria na hadhi za wachezaji ili kupatiwa ufumbuzi.
Miongoni mwa mambo ambayo yameonekana kama ni mkanganyiko ni kujitokeza kwa majina ya baadhi ya wachezaji katika orodha ya wachezaji wa klabu mbili.
Juu ya mikanganyiko iliyojitokeza Oseah amesema Simba imewasilisha fomu mama na mkataba wa mlinzi wake wa zamani Kelvin Yondani bila ya kuambatanisha fomu ya usajili ya mlinzi huyo ambapo kwa ujumla Simba imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji 28.
Kwa upande wa klabu ya Yanga ambayo ilimtumia mlinzi Yondani katika michuano ya Kombe la Kagame wamewasilisha kila kitu ikiwemo fomu mama, fomu ya usajili wake pamoja na mkataba wa mlinzi huyo aliyehamia klabu hiyo kwa mbinde toka Simba na wakiorodhesha jumla ya majina ya wachezaji 28.
Wakati hayo yakiwa hivyo nayo Azam fc imewasilisha tff jina la kiungo Ramadhani Chombo Lidondo pamoja na mkataba wake ndani ya klabu hiyo ilhali Simba wakiwasilisha vielelezo vyote muhimu ikiwemo fomu mama, fomu ya usajili na mkataba wake ndani ya klabu hiyo msimu huu.
Kwa upande wa ligi daraja la kwanza ni vilabu vitano tu vilivyowasilisha majina ya usajili wao wa wachezaji kati ya vilabu 24.
Katibu huyo wa tff Oseah amesema kwasasa inasubiriwa kamati ya Katiba,sheria na hadhi ya wachezaji chini ya mwenyekiti wake Alex Mgongolwa kuketi na kuamua juu ya hayo kwa kuwa kanuni ziko kimya juu ya hayo.
SIKILIZA HAPA.


1 comment:

  1. Kuna matatizo sana pale TFF.Vilabu vya Simba na Yanga wanapewa inside information na TFF offices na cha ajabu hakuna anayehoji kuwa ni vipi Simba au Yanga wawe na informanation za ndani za mchezaji wa timu nyingne?Hatuwezi kufika hata siku moja.

    ReplyDelete