Ngasa akikabidhiwa jezi ya Azam wakati akijunga nayo |
Mrisho Ngasa mwenye mpira |
Rockersports
imefanya jitihada ya kufanya utafiti kwa kutumia vyanzo vikuu vinne juu ya
taarifa hiyo ili kujiridhisha juu ya zoezi hilo la kukamilishwa kwa taratibi za
uhamisho wa Ngasa kwa mkopo kunako klabu ya Simba.
Rockersports
imeongea na pande zote mbili za mkataba huo yaani Simba na Azam, kisha
ikaelekea upande wa kamati ya sheria, hadhi na wachezaji ya shirikisho la soka nchini TFF kujua
hali ikoje inapotokea kuwepo na jambo kama hilo ambalo kimsingi muda wa kawaida
wa usajili umeshamalizika na kipindi kinachoendelea ni cha kuidhinisha
wachezaji wa mikopo.
Kama hiyo
haitoshi Rockersports ikafanya mazungumzo na Ngasa mwenyewe juu ya hilo kupata
ukweli hivi ni kweli anaelekea kucheza soka timu ya Simba?.
Ukweli wa
mambo uko hivi, kwa utaratibu mchezaji kucheza soka katika timu yoyote ni
makubaliano ya pande zote tatu, kwa maana ya timu anayotoka ,anayo kwenda na
mchezaji mwenyewe jambo ambalo halikufanyika zaidi ya Simba kutangaza offer ya
milioni shilingi 25 kwa ajili ya Ngasa na kukubaliana wenyewe bila ya saini ya
mchezaji, je taratibu zimekamilika?
Pili katika
makubaliano hayo kuna jambo la maslahi ya mchezaji ikiwemo mshahara na stahili
nyingine kule anako elekea kucheza soka lazima kukubaliana jambo ambalo
halikufikiwa.
Tatu ridhaa
ya mchezaji mwenyewe kama timu anayo pelekwa inamfaa ama la, kwa Ngasa hilo
anaonekana hayuko radhi nalo.
Azam watake
wasitake Ngasa ni mchezaji wao ana mkataba na klabu yao, hivyo ni vema
wakatumia busara kuliko hasira kwa yale yanayo fanywa na mchezaji huyo.
Mapenzi ya
Ngasa kwa Yanga ni jambo la kawaida kwa mtu yoyote kupenda jambo au kitu fulani,
huwezi kuzuia ni vema mkafuata taratibu za kumuuza kuliko kama ambavyo
inavyoendelea sasa.
Akiongea na
Rockersports Ngasa anasema hizo taarifa anazisikia tu lakini hajapewa taarifa
rasmi na uongozi wa klabu yake na kama kuchezea Simba basi ni bora akae msimu
mzima bila kucheza soka kwani thamani yake haijashuka kiasi kufikia milioni 25 wakati kuna timu zimetoa offer zaidi ya hiyo.
Namnukuu
Ngasa
“Simba ni
timu nzuri kubwa na sina matatizo nayo,lakini, utaratibu huu sijaupenda, ningehusishwa na mimi
katika mazungumzo yao lakini mimi sijui lolote nasikia tu”
Kuna mengi nyuma ya pazia,
fikiria juu ya kauli yake hiyo.
Katika siku za hivi karibu hususani baada ya michezo ya kombe la Kagame kumeibuka hali ya sintofahamu hususani juu ya hatma ya Mrisho Ngasa ndani ya klabu yake ya Azam hasa baada ya mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka
Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga na kushangilia bao la pili
katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akikimbilia upande wa mashabiki wa Yanga.
Kitendo kile kilizua hali ya sintofahamu ndani ya benchi la ufundi, viongozi na hata wamiliki wa klabu hiyo kwanini kafanya hivyo.
Sikatai kuwa linaweza kuvuruga utulivu wa akili ya mpenda soka, lakini sidhani kama linaweza kuifikisha klabu hiyo kufanya maamuzi ya kumuuza kwa style hii.
Ikumbukwe kuwa Ngassa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Azam FC,
akitokea Yanga miaka miwili iliyoipita kwa dau la Sh. Milioni 55.
Taarifa
Yanga imewasilisha offer ya shilingi milioni 50 Azam kutaka kumrejesha Ngasa Jangwani lakini Azam wanasema offer ya Yanga ilichelewa ndio maana wamekubali offer ya Simba ya milioni 25 , hivi kweli inaingia akilini wakati muda wa usajili wa wachezaji kwa mkopo haujafikia ukingoni kusema offer ya Yanga imechelewa?
karibu tujadili
ReplyDelete