FIFA yataja jila la mpira wa kombe la
dunia "Brazuca"
Bodi ya
utawala ya shirikisho la soka duniani FIFA imetangaza "Brazuca" kuwa
ndio jina rasmi mpira utakao tumika katika fainali za kombe la dunia 2014.
Jina hilo
limepigiwa kura na kupitishwa kwa asilimia 70% na kuizidi mipira ya Bossa Nova na Carnavalesca,
hii ikiwa ni taarifa ya FIFA iliyotoka jumapili.
"Neno
hilo hutumiwa na wabrazil kuelezea fahari ya maisha ya kibrazil. Wakielekeza hilo
katika soka limeelezea kuwa hamu ,fahari na nia nzuri ".
Kwa mujibu
wa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke kura hizo zina maanisha kuwa kwa mara ya
kwanza mashabiki wanajihusisha moja kwa moja na kutaja jina la mpira wa kombe
la dunia.
Amenukuliwa akisema
"nina
hakika kuwa mpira wa Brazuca utakuwa unaingia katika historia kama ilivyokuwa
kwa mipira mingine ilikuwa na majina makubwa duniani kama ilivyokuwa kwa Tango nchini
Argentina mwaka 1978 na Azteca nchini Mexico mwaka 1986,".
FIFA imesema
mpira huo ulikuwa bado unaendelea kuimarishwa na kujaribiwa katika uzinduzi
rasmi utakao fanyika kabla ya fainali za kombe la dunia 2014.
Zenit St Petersburg yamsajili Hulk na
Witsel kwa pauni million £64
Mshambuliaji
wa Kibrazil Brazil Hulk, ambaye alikuwa katika mazungumzo na Chelsea mwezi May,
amejiunga na Zenit St Petersburg akitokea Porto kwa ada ya uhamisho ya pauni
milioni £32.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 26 ameingia mkataba wa miala miatano na mabingwa hao
wa Russian, ambao wako chini ya meneja Luciano Spalletti.
Zenit pia
imekamilisha kumsajili kiungo Axel Witsel, mwenye umri wa miaka 23, akitokea Benfica
kwa ada kama hiyo.
Hulk amekaririwa
akisema
"nilikuwa
mwenye furaha Ureno na ninataka kuwa mwenye furaha hata hapa Russia pia."
Zenit St
Petersburg iko katika jitihada za kuimarisha kikosi ambacho kinawinda akina Bruno
Alves na Danny. Pia walikuwa wakihusishwa na kumtaka nyota wa Manchester United,
Nani.
Witsel naye
kama ilivyo kwa Hulk, naye ameingia mkataba wa miaka mitano.
Kocha muasisi nchini Misri Mahmoud el
Gohary amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74
Kocha
mkongwe nchini Misri Mahmoud el Gohary amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74
baada ya kupatwa na ugonjwa wa kupooza ubongo akiwa Jordan.
Taarifa
kupitia shirika la habari la MENA zimesema El Gohary anaangaliwa kama ni mtu
muhimu na alama kubwa ya maendeleo ya soka nchini Misri ambapo aliwahi kuwa
kocha wa timu ya Taifa ya nchini hiyo maarufu kama Mapharaoh katika fainali ya
kombe la dunia mwaka 1990.
Katika
fainali hizo mbali ya umaarufu mikubwa nchini kwake alipelekea timu yake kupata
sare dhidi ya Uholanzi ya bao 1-1 yakiwa ni matokeo makubwa katika historia ya
soka la nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuingoza Misri katika fainali za mataifa
ya Afrika mwaka 1998 na kutwaa taji hilo.
Marekani yaisimamisha Falconets kombe la dunuia Wanawake FIFA U-20
Timu ya
taifa ya wanawake ya Nigeria Falconets ya wachezaji wenye umri chini ya miaka
20 imeshindwa kufikia fainali ya FIFA ya kombe la dunia ya U-20 kule Japan, baada
ya kulambwa kwa mabao 2-0 kwa mabingwa mara mbili ya fainali hizo Marekani
katika mchezo uliopigwa katika dimba la ‘Tokyo National Stadium’.
Mabao kupitia
kwa Morgan Brian na Kealia Ohai yalitosha kuwaumiza wanigeria ambao katika
fainali zilizo pita walikuwa washindi wa pili mika miwili iliyopita fainali
zilizo fanyika nchini Ujerumani.
Falconets walitawala
mchezo lakini walishindwa kutumia nafasi walizopata kwa kushindwa kupiga
mashuti langoni mwa adui.
Sasa
Marekani itakuwa inaingia katika mchezo wa fainali kwa mara ya tatu na watakuwa
wakicheza dhidi ya ama Ujerumani au wenyeji Japan.
Mchezo wa
fainali unatarajiwa kupigwa jumamosi katika uwanja wa taifa wa Tokyo National
Stadium, baada ya mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambao Nigeria watacheza
dhidi ya timu itakayo poteza katika mchezo kati ya Japan na Ujerumani.
No comments:
Post a Comment