KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 24, 2012

Hodgson amekubali kwa shingo upande kustaafu kwa John Terry timu ya Taifa na Messi anasema hana matatizo na Villa.


Hodgson amekubali kwa shingo upande kustaafu kwa  John Terry timu ya Taifa
Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson ameonyesha kusikitishwa kwake na hatua ya mlinzi wa kimataifa wa John Terry kustaafu soka la kimataifa lakini amesema hana budi kukubaliana na maamuzi yake.

Nahodha huyo wa Chelsea ameamua kuachana na soka la kimataifa jumapili usiku kuelekea katika kesi ya FA kusikiliza shauri dhidi yake la matumizi ya lugha ya kibaguzi dhidi ya mlinzi wa QPR Anton Ferdinand October mwaka jana huku akisema hakuna nafasi ya kuilinda tena nafasi yake katika timu ya Taifa.

Meneja huyo amemtakia kila la kheri mlinzi huyo katika utumishi wake pale Stamford Bridge na kutanabaisha kuwa taarifa hizo amezipokea kwa mshtuko sana.
amenukuliwa akisema
"ningependa kumshukuru John Terry kwa namna alivyo wajibika katika taifa lake la England tangu nianze kazi ya umeneja, kwa kweli nimesikitishwa kumkosa mchezaji mwenye uzoefu na uwezo wa kimataifa kama John"
"ningependa kumtakia kila la kheri akiwa na klabu yake ya Chelsea."
Kwa upande wa taarifa ya FA pia imeendana na maneno ya Hodgson wakati ambapo Terry akiwa na rikodi ya kuwa nahodha katika kikosi cha Three Lions mara mbili ndani ya kipindi cha mizengwe dhidi yake.

Taarifa ya FA imesomeka,
"kufuatia kutangaza kwake kutoka katika timu ya taifa ya  England, FA ingependa kumshukuru John Terry kwa jitihada zake katika timu ya Taifa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

"katika kipindi cha uchezaji wake michezo 78 aliyo itumikia timu ya Taifa John mara zote alijitoa kikamilifu katika timu."
 
Messi akanusha kuwa na matatizo na Villa

Lionel Messi amekanusha kuwa na matatizo na David Villa baada ya kutoleana maneno katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Granada mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga uliopigwa jumamosi, malumbano ambayo yalinaswa na vyombo vya habari.
Katika mchezo huo uliopigwa Camp Nou, kabla ya mapumziko na matokeo yakiwa 0-0, Messi, alikwaruzana na Villa baada ya kuharibu shambulizi zuri wakiwa ndani ya eneo la hatari la Granada ambapo alionekana Messi akimlalamikia Villa kwa kushindwa kumpasia pasi ya mwisho mapema akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.

Television ya nchini Hispania ilirudia tukio hilo mara kadhaa kutoka kona mbalimbali za uwanja jambo ambalo lilionekana kama tukio kubwa kutokea baina yao.

Hata hivyo   Messi amesisitiza kuwa hakuna haja ya kulikuza tukio hilo ambalo limesha pita na kudharau jambo hilo.

"kitu kama hicho hutoke katika mchezo, ni kitu cha kawaida, utataka kufunga goli la kwanza na baadaye kila kitu kinakuwa kawaida . yanatoke katika mazoezi lakini watu hawaoni hilo hivyo ni kitu cha kawaida"

"sina tatizo na ‘el Guaje’ yaani Villa, ni kinyume na mnavyo fikiria. Historia yangu na yeye iko poa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo tuko poa, usitafute matatizo sehemu ambayo hakuna hilo, tulikasirikiana kwasababu tulitaka kufanya vizuri na mazingira yanaweza kukufikisha hapo."

No comments:

Post a Comment