KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 25, 2012

Champions League ni muhimu kuliko ligi :Arsene Wenger na Barcelona wakata rufaa juu ya kifungo cha Mascherano.



Champions League ni muhimu kuliko ligi :Arsene Wenger
 Arsene Wenger amesema michezo ya kuwania kufuzu vilabu bingwa Ulaya ni muhimu zaidi ya kushinda mataji ya FA na League Cup.
Washika mitutu hao ambao hawajawahi kushinda taji lolote tangu mwaka 2005, kwasasa wako ndani ya kinyang’anyiro hicho kwa miaka 15 mfululizo.
Akikaririwa meneja Wenger anasema
"kuna mataji matano kushindania, la kwanza ni ligi, la pili vilabu bingwsa , la tatu ni kampeni ya kufuzu vilabu bingwa, nne ni na tano ni kushinda taji la ligi"
Akaongeza kwa kusema
"nasema hivi kwasababu kama unataka kuwapendeza wachezaji bora, hawatakuuliza kama umeshinda taji la ligi, wanauliza kama unacheza vilabu bingwa ulaya."
Wenger alikuwa wa mwisho kuongea katika kikao cha wanahisa ambacho kimsingi kilimpongeza.
Hata hivyo aliomba radhi kwa matokeo ya jana ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Schalke ambacho kilifuatia kichapo cha ligi kuu toka kwa Norwich.
"samahani kwa usiku wa jana "
"najua haikuwafurahisha mashabiki"
Hotuba ya Wenger kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni kutuliza hali ya mambo ilivyo juu ya matokeo ya timu yake.

Barcelona wakata rufaa juu ya kifungo cha Mascherano.
Barcelona imetangaza kupitia mtandao wa klabu yao kuwa imekata rufaa katika kamati ya rufaa ya ligi kuu ya nchini Hispania La Liga baada ya Javier Mascherano kupewa kibano cha kusimama mchezo mmoja kutokana na kuonyeshwa kadi nyekundu wiki iliyopita.

Muarjentina huyo alikutana na adhabu hiyo katika mchezo ambao Barca walichomza na ushindi wa mabao  5-4 dhidi ya Deportivo La Coruna jumamosi baada ya kutanguliziwa kupewa kadi mbili za njano na mwamuzi Jose Paradas.

Barca imewasilisha rufaa hiyo dhidi ya taarifa ya mwamuzi iliyowasilishwa baada ya mchezo, na sasa baaada ya kupitia taarifa iliyoelezea adhabu hiyo wakawasilisha rufaa nyingine dhidi ya kamati hiyo ya rufaa.

Catalans wanaimani ya kwamba watakuwa na Mascherano katika mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Rayo Vallecano, akiwa kama mlinzi wa kati wakati huu ambapo Carles Puyol na Gerard Pique wakiwa bado hawaja rejea kikosini kutokana na kukabiliwa na majeraha.

Mascherano, mwenye umri wa miaka 28, tangu kuanza kwa msimu huu, ameitumikia timu yake michezo 12.

No comments:

Post a Comment