Cristiano
Ronaldo, Kaka na Sergio Ramos wameelezea kufurahishwa kwao na ushindi wa Real
Madrid wa mabao 4-1 ugenini dhidi ya Ajax na kusema kuwa wanaamini wataibuka na
ushindi katika dimba la Camp Nou dhidi ya Barcelona katika mchezo ujao.
Ronaldo alikuwa
shujaa wa kikosi cha Jose Mourinho akipiga ‘hat-trick’ wakati ambapo Ricaldo Kaka
na Sergio Ramos wakianza katika mchezo licha ya kwamba hawakuwa katika kiwango
kizuri.
Akiongea na
kituo cha television cha Canal+, Ronaldo amenukuliwa akisema
"nimefurahi
kwasababu tumeshinda na tumecheza vizuri, kwangu mimi kufunga magoli matatu na
jambo kubwa.
"tumecheza
soka letu kamili na ni jambo muhimu kuongeza kujiamini kuelekea katika mchezo
ujao dhidi ya Barcelona.
"ni
muhimu kuondoka na mpira nyumbani lakini muhimu zaidi ni timu kwasababu bila
wao nisingeweza kufunga magoli."
Barcelona inaweza
kuongoza kwa kuongeza points 11 endapo itafanikiwa kuifunga Los Blancos katika
mchezo wa jumapili, lakini Ronaldo anaamini kuwa kikosi chao kinaweza kuibuka
na ushindi wanao utaka.
"nina
matumaini kuwa tutapata matokeo mazuri katika eneo gumu la Camp Nou. Wana kikosi
kizuri lakini hakutakuwa na utofauti mkubwa".
Wakati hayo
yakiwa hivyo, licha ya kwamba amekuwa si chaguo la kocha lakini vilevile akiwa
katika matatizo na kocha wake, Sergio Ramos hapo jana alianzishwa katika kikosi
cha kwanza na amenukuliwa akisema anaamini wataendelea na mwendo wao mzuri.
"matatizo
na Mourinho yamekwisha, na ninafuraha kwa ushindi katika mchezo wa ligi ya
mabingwa, ushindi ambao ni muhimu katika timu".
"ulikuwa
ni ushindi muhimu dhidi ya timu ngumu, lakini sasa tunaangalia mchezo wa La
Liga.
"Clasico
inakuja na siku zote ni ‘special’. Tunapaswa kuendelea na mwendo huu na kupata
points zaidi katika ligi"
ROBERTO MANCINI AKERWA NA UVIVU WA WACHEZAJI WAKE
Roberto
Mancini ameonya kuwa Manchester City inatakiwa kupigania kila mchezo kama
wanataka kweli wanataka kushindana katika ligi ya mabingwa kauli ambayo ameitoa
kufuatia kutapa sare ya bahati dhidi ya Borussia Dortmund.
Mabingwa hao
wa ligi kuu ya England walikuwa katika kiwango kibovu katika sehemu kubwa ya
mchezo wao dhidi ya mabingwa mara mbili wa Bundesliga , lakini hata hivyo
wakafanikiwa kupata sare iliyotokana na mpira wa penati uliopigwa na Mario
Balotelli na hivyo kuzima bao la utangulizi la Marco Reus.
Itakumbukwa City
iliondolewa katika hatua ya makundi ya michuano hiyo msimu uliopita na sasa
inaonekana kuwa katika hatari kama ya mwaka jana baada ya kuambulia point moja
baada ya kushuka dimbani mara mbili.
Mancini ametupia
lawama kikosi chake kwa kucheza soka bovu na kusema kikosi chake kimekosa
kujituma na kukosa pia hamu ya ushindi na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kucheza
soka lisilo vutia.
Akinukuliwa na
Sky Sports amesema,
"hatukucheza
vizuri kwakuwa Borussia Dortmund walicheza vizuri kushinda sisi. Nadhani niwazuri
zaidi kuliko sisi, kama tunataka tunataka kucheza katika kiwango cha juu cha
ligi ya mabingwa ulaya, tunapaswa kukimbiza zaidi ya tulivyo fanya usiku huu.
"tunapaswa kukimbia, kupigania kila mpira. Sio
tu kucheza pasi nzuri katika ligi ya ligi ya mabingwa ni zaidi ya hapo. Michuano
hii ni ya kiwango kingine.


No comments:
Post a Comment