KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 3, 2012

ILI KUNUSURU KITUMBUA CHAKE, ALLEGRI ATAKA VIJANA WAKE KUBADILIKA KWANI WAKUBWA WA MILAN WANATAKA USHINDI.


Meneja wa AC Milan Massimiliano Allegri anaamini kikosi chake kina kila sababu ya kuimarika zaidi katika kipindi hiki wakiwa wanaelekea katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya usiku huu dhidi Zenit St Petersburg.

Milan ambao wako katika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ya soka ya Italia maarufu kama ‘Serie A’, meneja wake ambaye yuko katika shinikizo kubwa la matokeo mabaya, anadhani vijana wake wanatakiwa kufanya jitihada zaidi ili kuwaadhoofisha wapinzani wao.

Amenukuliwa akisema,
"tunapaswa kudhihirisha kuwa tunatimu nzuri yenye ufundi mkubwa. Lakini pia bado kuna mengi ya kujifunza ili kuimarika zaidi".

"Zenit ni timu nzuri. Soka la Urusi ni kubwa. Uwepo wa Hulk na Axel Witsel imeonyesha kuwa kuwa wamepiga hatua kubwa mbele.

"Luciano Spalletti ni kocha mzuri. Ameshinda Coppa Italia akiwa na kikosi cha Roma, na ameshinda ligi hapa Urusi. Timu zake mara nyingi huwa zinacheza soka zuri."

Wakati huohuo mmiliki wa Milan Silvio Berlusconi amekanusha taarifa za fununu kuwa alikuwa anafikiria kufanya mabadiliko katika nafasi ya makamu wa Rais inayoshikiliwa na Adriano Galliani kutokana na matokeo mabovu ya timu yake.

Amenukuliwa akisema,
"natumia fursa hii kukanusha taarifa hizo, na ninaweka wazi juu ya ninavyo mkubali na nilivyo na imani na Adriano Galliani, kumekuwepo na baadhi ya taarifa kuhusiana na Milan hizi taarifa ziko mbali na ukweli.

"ni mmoja kati ya watu muhimu katika mchezo, na ni rafiki yangu kwa zaidi ya miaka 30 nina muheshimu sana."

No comments:

Post a Comment