Inter yampiga marufuku Sneijder kuchati kwenye
mtandao wa Twitter.
Klabu ya Inter
Milan ya Italia imempiga marufuku kiungo wake Wesley kutumia mtandao wa kijamii
wa Twitter.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akitumia mtandao huo wa
kijamii kuwasiliana kwa muda mrefu na watu zaidi ya milioni moja licha ya kwamba hajakutana na
jambo lolote baya la kimtandao.
Mke wa
kiungo huyo ameandika kupitia mtandao wa twitter kuwa mumewe si muda
mrefu ataacha kuchati kwa kutumia mtandao huo.
Ameandika mtandaoni
kuwa,
“muwe wangu @sneijder101010
si muda mrefu ataacha kuandika kwenye mtandao wa Twitter,”.
“haya ni
maamuzi ya klabu yake. Wamesema kuwa amekuwa hana msaada tena na timu. Nasikitika
kwasababu amekuwa akijituma kwa ajili ya timu kwa moyo wake wote.
“siyo kawaida lakini hakuna tabu. Tusubiri tuone
jinsi atakavyo rejesha morari ya ushindi katika klabu yake.”
Sneijder amekuwa
nje ya uwanja kwa muda sasa akisumbuliwa na msuli mamumivu aliyoyapata katika
mchezo dhidi ya Chievo mwezi Septemba.
Juventus wanamtaka Lewandowski
Mabingwa wa
soka nchini Italia Juventus imejiweka katika mkao wa kumnasa Robert Lewandowsky
licha ya kwamba itawagharimu mapesa mengi kunasa saini yake.
Mshambuliaji
huyo wa Borussia Dortmund ameendelea kuwa muhimu katika klabu hiyo ya nchini
Ujerumani tangu ajiunge nayo mwaka 2012 akitokea Lech Poznan na kiwango chake
hakijashuka tangu wakati huo akiwa nchini Italia.
Juve
ilimtuma kijumbe wake kumfuata mshambuliaji huyo katika mchezo ambao Dortmund ilikwenda
sare ya bao 2-2 dhidi ya Real Madrid jumanne iliyopita ambapo Lewandowski hakuwa
katika kiwango kizuri katika mchezo huo kiasi cha kumridhisha kijumbe huyo.
Hata hivyo ni kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 si kwamba atapatikana kwa
bei ya chini endapo Juventus watakuwa tayari kutaka huduma yake.
Dortmund haina
mpango wa kumuweka sokoni Lewandowski, lakini huenda kama ofa ya klabu hiyo
itafikia euro milioni €35 basi inaweza kumshawishi mchezaji huyo kuondoka
katika klabu yake ya sasa.
Nyota huyo wa kimataifa wa Poland kwasasa ana mkataba na Signal
Iduna Park mpaka June 2014 lakini pia huenda klabu yake ikamuongezea muda wa
kuendelea kusalia katika klabu hiyo.
Real Madrid ndiyo klabu yenye academy
ya mafanikio ulaya nzima.
Mlinzi wa zamani
wa Real Madrid Francisco Pavon amesema kuwa Real Madrid ndiyo klabu yenye mfumo
mzuri katika kujenga vijana kuliko kituo chochote cha kujenga vijana kikiwemo kile cha Barcelona cha ‘La Masia’.
Kauli ya
Pavon imekuja baada ya hivi karibuni kuibuka ukosoaji mkubwa kufuatia Santiago
Bernabeu kusitisha kuchukua wachezaji kutoka katika Academy yao, lakini Pavon ambaye ni zao la academy hiyo akipinga
ukosoaji huo.
Amenukuliwa akisema,
"kila
mtu anataka kuongelea juu ya academy hii, mimi naamini kuwa academy ya Madrid ndio
bora nchini Hispania na ulaya nzima kwa ujumla"
Pavon pia
amejibu kauli ya mkurugenzi wa Andoni Zubizarreta aliyesema kuwa Madrid inaogopa
kutimiza ahadi yao kwa vijana.
Cavani: Nataka kuvunja rekodi ya Maradona Napoli.
Edinson
Cavani anaota ndoto ya kufikia na hata kuipita rikodi ya ufungaji mabao ya Diego
Maradona aliyoweka katika katika klabu ya Napoli.
Mwasisi huyo
wa soka duniani na nchini Argentina alifunga magoli 115 katika kipindi cha miaka saba
alicho chezea klabu hiyo ambapo Cavani anasema atafikia rikodi ya mkongwe huyo muda
si mrefu ambapo kwasasa mkongwe amefikisha umri wa miaka 52.
Cavani nyota wa zamani wa Palermo alifunga magoli manne katika mchezo ambao Napoli ilishinda
mabao 4-2 dhidi ya Dnipro Dnipropetrovsk hapo jana na kufikisha jumla ya mabao 79.
Amenukuiliwa
akijiuliza kwa kusema,
"rikodi
ya Maradona ya ufungaji? Naikaribia taratibu nitaifikia ".
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 ameshafunga jumla ya mabao 13 katika michezo 13 aliyochezea
timu yake msimu huu.
No comments:
Post a Comment