Klabu ya Simba imekanusha tuhuma nzito zilizotolewa na klabu ya Azam juu ya tuhuma za Simba kutoa rushwa kwa baadhi ya wachezaji wake ambao klabu hiyo hapo jana ilitangaza kuwasimamisha.
Wachezaji waliokumbwa na tuhuma hizo ni pamoja Erasto Nyoni, Deogratius Munishi 'Dida' na Said Moradi ambao kimsingi wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo kufanyika.
Azam jana kupitia kwa afisa habari wake Jafari Iddi Maganga ilitoa taarifa za kuwatuhumu wachezaji hao kuwa walihusika kufanya vitendo hivyo katika mchezo dhidi ya Simba licha ya kwamba Dida na Erasto kutokucheza katika mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa mabao 3-1.
Hii leo akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu hiyo afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amekanusha tuhuma za Simba kuhusika na rushwa kwa wachezaji hao na kwamba wao kama Simba wako tayari kutoa ushirikiano kwa Azam katika kuchunguza juu ya ukweli wa tuhuma hizo.
Kamwaga amesema klabu ya simba haijawahi kufanya mkutano wowote au kumtuma yoyote kwenda kufanya jambo hilo la rushwa kwamba Simba ni miongoni mwa vilabu vinavyopinga mambo ya rushwa michezoni.
Ameitaka Azam kuilipeleka suala hili katika vyombo vya dola na kwamba wako tayari kutoa ushirikiano.
Amesema simba haipingi juu ya kile kilichoelezwa na Azam isipokuwa wanaomba taarifa hizo zifikishwe katika dola ili ukweli ubainike kupitia mkondo hisika.
Wakati huohuo shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha juu ya kupokea taarifa za tuhuma za rushwa kwa wachezaji wa Azam.
Katibu wa TFF Angetile Oseah amesema TFF imepokea taarifa ya klabu hiyo inayo arifu juu ya kuwasimamisha wachezaji wao watatu akiwepo Dida, Moradi na Nyoni.
No comments:
Post a Comment