KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 9, 2012

TENGA AMPA RIDHIWANI KIKWETE RUNGU LA KUWAMALIZA CONGO BRAZAVILLE.

Rais wa shirikisho la kandanda nchini Tanzania Leodigar Chila Tenga ameunda kamati maalumu itakayokuwa chini Ridhiwani Kikwete kwa lengo la kuhakikisha timu ya taifa ya vijana ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys inafuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.
 
Kamati hiyo pia itakuwa na jukumu la kuwezesha umma wa watanzani unafahamu juu ya umuhimu wa mechi ya mwisho ya Serengeti Boys dhidi ya Congo Brazzville itakayo fanyika kati ya tarehe 16 na 18.

Kamati hiyo itakuwa na wajumbe wengine kadhaa akiwemo mwenyekiti wa soka la vijana alhaji Ahmed Msafiri Mgoyi, Nasor Bin Slum, Ahmed Seif, Abubakar Bakheresa, Angetile Oseah, Kassim Dewji, Abdalah Bin Kleb, Salim Seif na Henri Tandau.

Kamati hiyo imeanza kukutana hii leo kwa lengo la kupanga mikakati ya kukusanya fedha ili kufanikisha ushindi katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Congo Brazaville.

Serengeti kwasasa inaendelea vizuri na maandalizi yake chini ya kocha wake Jacob Michelsen akisaidiwa na kocha mzalendo Jamhuri Kihwelu 'Julio'.

Ili Serengeti ifuzu fainali hizo italazimika kupata ushindi wa kishindo katika mchezo wake wa kwanza hapa nyumbani kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye.

No comments:

Post a Comment