Mashindano ya klabu bingwa ya taifa 2012 yaliyokuwa yaanze
Kufanyika kuanzia tarehe 26-30/11/2012 yamesogezwa mbele hadi 29/01-03/02/2013
kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu zilizopelekea mashindano hayo kusogezwa mbele kubwa ni
hadi tunapotoa taarifa hii katika vyombo
vya habari hakuna timu iliyokamilisha taratibu tulizoziweka za kuweza kusaidia
kukamilisha mashindano hayo kwa ufanisi.
Kwani katika barua ya taarifa ya
mwaliko wa kushiriki katika mashindano BFT iliagiza kufikia tarehe 15/11/2012
timu zote ziwe zimethibitisha ushiriki wao ikiwa pamoja na kuwasilisha majina
na picha za mabondia na viongozi watakaoshiriki
katika mashindano hayo na kulipa ada ya ushiriki ya Tsh. 200,000/=.
Hadi leo hakuna hata timu moja iliyokamilisha utaratibu huo
kwa nia ya kupanga mashindano vizuri ili yawe na hadhi ya taifa kwa kuzingatia
sheria za chama cha ngumi cha dunia (AIBA)
Sababu kama hizi mara nyingi zimesababisha mashindano mengi
kuyaendesha katika kiwango cha chini na lawama nyingi kuelekezwa kwa BFT bila ya
kufahamu sababu za msingi za kusababisha kutokea hivyo.kitu ambacho tungeweza
kuepukana nacho kama tutafata taratibu
tulizojiwekea.
Kwani kwa kufanya hivyo tungejua mapema idadi ya washiriki ili kupanga mipango
halisi ya Kufanyika kwa mashindano.
Aidha kozi ya waamuzi iliyokuwa ianze tatehe 11-30/11/2012
imeshindwa Kufanyika kutokana na wanafunzi walikuwa wameomba kujiunga na kozi
hiyo kushindwa kufika kwa wakati na kushindwa kukamilisha malipo ya kujiunga na
kozi kwa wakati.
Kutokana na majukumu mengine iliyonayo BFT kozi hiyo sasa itafanyika
kuanzia tarehe 15/01-04/02/2013 na mazoezi ya vitendo yatafanyika katika
mashindano ya klabu bingwa.
Kwa sasa BFT nguvu kubwa inaweka katika usajiri kwa makocha
.waamuzi ,mabondia, madaktari katika data base za chama cha ngumi cha dunia
(AIBA) ili wengi watambulike kwa ajili ya kujiunga na mashirikisho ya ngumi za
kulipwa ndani ya ngumi za ridhaa (AIBA
PRO BOXING).
Makore Mashaga
KATIBU MKUU (BFT)
No comments:
Post a Comment