KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, December 18, 2012

MZEE FERGUSON ANASEMA SAFU YAKE YA USHAMBULIAJI YOTE SASA MOTO. WAARABU WA PSG WAANZA VURUGU MADRID, WATANGAZA KUCHUKUA KUKU NA MAYAI YAKE.


MENEJA wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekiri kuwa ujio wa Robin van Persie umeimarisha uwezo wa kikosi chake hususani katika eneo la ushambuliaji.
Akiwa tayari ameshatupia wavuni jumla ya mabao 15 , mshambuliaji huyo raia wa uholanzi hajafanya makosa ya kusubiri kujenga jina Old Trafford, huku meneja wake Ferguron mbali ya kumpongeza yeye, lakini pia amekiri kuwa kwa ujumla kikosi kizima cha United kimebadilika kiuwezo kiasi kupelekea washambuliaji wote kuonyesha makali yao.
 
Amenukuliwa Sir Alex akisema,

Eneo la ushambuliaji kwa hakika limeimarika tangu kujiunga kwa Van Persie na kwakweli ametia nguvu  akifunga magoli 14 kabla ya ushindi wetu wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland mpaka sasa"

"Chicharito sasa ana magoli tisa, Rooney magoli saba, nadhani nafikiri tuna magoli 43 kama timu jambo ambalo ni idadi ya juu katika kipindi hiki cha mwaka"



Sir Alex akazidi kwenda mbele zaidi kwa kutoa maoni yake akilinganisha kipindi hiki cha ujio wa Van Persie na mwaka 1992 wakati wa ujio wa Eric Cantona, akisema kila mchezaji anahitaji mazingira ya aina yake kuzoea mazingira

"Van anafanana kisifa na Eric kwa nyakati za ujio unapo zungumzia umri na ukomavu"

"alikuwa na kipindi kizuri sana wakati wa utumishi wake  Arsenal hivyo hakuna haja ya kurubiri kuzoeamazingira ya Premier League.

"ametokea katika klabu kubwa na amekuja katika klabu kubwa na amejiamarisha kumataifa, mambo yote haya ni muhimu kwetu"



PSG imethibitisha kumtaka Mourinho na Cristiano Ronaldo.
 Sheikh Bin Abdulrahman Al-Thani ameweka wazi kuwa Paris Saint-Germain inawataka Cristiano Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho kutoka Real Madrid.
Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi huko nyuma aliwahi kukaririwa akikanusha taarifa kuwa kigogo hicho cha ligi kuu ya nchini Ufaransa Ligue 1 kuwa kilikuwa na mpango wa kumsainisha kocha wa Madrid na Ronaldo lakini mtu wake wa upande wa pili ameibuka na kusema wazi kuwa ili lengo la kutwaa ligi ya vilabu bingwa Ulaya litimie basi lazima watafute watu muafaka.
Akiongea na Canal Football amesema,
"Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho ni miongoni mwa malengo yetu hapa Paris Saint-Germain".
"PSG ni miongoni mwa klabu kubwa duniani. Na hivyo moja ya malengo yetu ni kushinda taji la vilabu Ulaya.
"ni klabu kubwa Ufaransa, hivyo lengo ni kuwa klabu bora Ulaya na duniani kwa ujumla"

No comments:

Post a Comment