KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 19, 2012

USAJILI WA AZAM FC, PIGA MAKOFI TAFADHALI

Katika kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili na mashindano ya Afrika Azam FC imefanya usajili wa wachezaji nane wapya katika kipindi hiki cha dirisha dogo
 
Azam FC ambayo ilikuwa na wachezaji wanne wa kimataifa kufuatia George Odhiambo"blackberry" kuondolewa mapema kutokana na utovu wa nidhamu pia iliwapunguza wachezaji Ibrahim Shikanda na Joseph Owino na hivyo kuwa na nafasi tatu za kimataifa
Hatimaye sasa Azam FC imejaza nafasi hizo kwa kuwasajili Jockins Atudo, beki wa kati wa Harambee Stars na klabu ya Tusker FC, Kiungo mshambuliaji wa Harambee Stars na Sofapaka Humphrey Mieno pamoja na mshambualiaji na mchezaji bora wa mashindano ya CECAFA Challenge Cup Brian Umony.
Pia Azam FC imemsajili kinda anayeshika nafasi ya pili kwa kufunga magoli ligi kuu akiwa na magoli sita nyuma ya Kipre Tchetche na Didier Kavumbangu wenye magoli nane kila mmoja Seif Rashid Abdallah toka Ruvu Shooting Stars
Kama hiyo haitoshi Azam FC ambayo ilikuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup mwaka huu kwa kuwa na wachezaji 11, imemewarudisha walinzi Malika Ndeule na Omary Mtaki waliocheza katika vilabu vya African Lyon na Mtibwa Sugar katika mzunguko wa kwanza.
 
Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pia imemsajili mlinzi wa kati wa Tanzania Prisons David Mwantika. Na kumsajili kwa mkopo winga wa Simba Uhuru Selemani.
 
Usajili huu umesimamiwa na mwalimu Stewart Hall mwenyewe ambaye anaamini maboresho haya yatakiongezea nguvu kikosi cha Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza januari 20.

Kwa mtanzania wa kweli anayejua na kufuatialia mambo ya soka la ukanda wetu wa Afrika Mashariki na kati na nyumbani kwa umakini, atakuwa amekubaliana waziwazi na Stewart kuwa amefanya usajili makini kwa lengo la kufidia mapungufu ya timu hiyo.

Itakumbukukwa baada ya Azam kuwasimamisha kazi wachezaji wake kadhaa kwa tuhuma za rushwa baada ya mchezo dhidi ya  Simba, swali lilikuwa ni namna gani timu hiyo kwa mara moja itaweza kuziba mapengo hayo yalioachwa na wachezaji muhimuj kabisa kikosini.

Wachezaji waliondolewa walikuwa ni pamoja na nahodha Aggrey Moris, mlinzi tegemezi wa pembeni upande wa kulia Erasto Nyoni, mlinzi mzoefu wa kati Saidi Moradi na mlinda mlango Deo Mushi 'Dida' ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa nguzo ya timu hiyo.

    Binafsi nampongeza kocha wa Kingereza Stewart kwa umakini wake huku akijua wazi kuwa Azam wanadhamana ya watanzania ya kuwawakilisha katika michuano mikubwa barani Afrika ya kombe la shirikisho, hongera Stewart.

Nina amini wengi tumeshuhudia michuano ya chalenji ya Kampala katika Luninga zetu na hakuna wakumdanganya mtu kuwa Umony, Atudo na Hamphrey Mieno kwamba hawakuonyesha soka la kuvutia katika michuano hiyo.

Uhuru Selemani na David Mwantika wadau wa kweli wa soka la Bongo lazima watakuwa wanawajua hakuna haja ya maelezo mengi, lakini pia hata Seif Rashid Abdalah wengi wanamjua hivyo tuseme kuwa Azam inastahili pongezi kwa kutumia vema nafasi ya usajili wa dirisha kuongeza nguvu iliyohitajika ili kufikia lengo. 
Vifaa vipya vya Azam Brian Umony mwenye jezi ya njabo na Jockins Atudo mwenye nyekundu wakati wa michuano ya Chalenji.
 Azam FC ipo jijini Kinshasa DRC ikijiandaa na mzunguko wa pili na mashindani ya kimataifa kwa kusaka uzoefu wa kucheza nje ya nchi na imeshacheza michezo miwili na timu za Dragons and FK Sharks ambapo ilitoka sare 1-1 mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili 0-2.
 
Azam FC inatarajia kurejea nchini December 26 ambapo itaelekea visiwani Zanzibar moja kwa moja kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo inayashikilia.

Rockersports inawatakia ziara njema huko Congo na mrudi salama Tanzania tayari kwa maandalizi ya ligi ili tuone vifaa hivyo vipya vikicheza katika muondo wa timu mpya kabisa.

No comments:

Post a Comment