Inavyo
onekana mara baada ya dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2013 kufunguliwa
mwezi January, hakutakuwa na uhaba wa upatikanaji wa vipaji.
Mwezi January
sasa umefika ambapo dirisha dogo la usajili litakuwa likifunguliwa tena barani
ulaya. Kumekuwepo na majina mengi
makubwa ambayo yamekuwa yakihusishwa na kutaka kuhama kutoka upande mmoja
kuelekea upande mwingine, ambapo vilabu vikubwa katika bara hilo la Ulaya navyo
vikihaha kusaka vipaji vipya.
Kwa msaada
wa mtandao wa Goal.com hebu tuangalie majina hayo yanayotajwa kuwa huenda
wakahama kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine mwezi huu wa January.
Wesley Sneijder, Inter
Kiungo
mchezeshaji huyo raia wa Uholanzi amekuwa hana nafasi tena katika kikosi cha
kwanza San Siro. Sneijder ametamka waziwazi kuwa itakuwa vema kwake kama
ataondoka katika klabu yake katika dirisha hili la usajili, kiasi kuviweka
vilabu vikubwa barani humo kukaa mkao wa kumsubiri.
Taarifa za
awali zinasema kuwa Sneijde ameshakubaliana katika mambo fulani ya msingi na klabu
ya Tottenham na kwamba mpango huo umefikia hatua nzuri ambapo pia kuna vilabu
kadhaa vya ligi kuu ya England vikimtamani kama vile Manchester City, Liverpool
na Manchester United.
Pia Anzhi
Makhachkala ya Russia pia iko katika mpango huo.
Demba Ba, Newcastle
Mshambuliaji
huyu ni raia wa Senegal ambaye amekuwa mfungaji mkubwa wa Newcastle, akiifungia
magoli 29 katika jumla ya michezo 54 aliyocheza klabu hiyo.
Ba, amevutia
vilabu vingi vikubwa ambapo Chelsea na Arsenal ni vilabu ambavyo kuna tetesi
zinasema wanamtaka Ba mwenye umri wa miaka 27,
Kuondoka
kwake kunaweza kumfanya meneja Alan Pardew kuwasajili Mathieu Debuchy na Loic
Remy.
Theo Walcott, Arsenal
Kwa hali ya
mambo ilivyo ni kwamba mkataba wa Theo Walcott katika klabu yake ya Arsenal uko
katika hali ya sintofahamu ambapo kwa kwasasa umekuwa unaangaliwa na vilabu
vingi vikubwa barani Ulaya wakisubiri majaaliwa yake.
Wakati
mkataba huo ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu, vilabu mbalimbali sasa
vimekodoa macho wakirubiri hatma yake mwezi January.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa England mwishoni mwa juma alipiga bao tatu “hat trick”
katika mchezo dhidi ya Newcastle ambayo kwa kweli imeongeza thamani yake katika
mpango wake ujao usajili wa nyongeza kama washika mitutu watashawishika
kumsajili tena Walcott na kwa vyovyote vile itakuwa ni busara kumsajili tena
kuliko kumuacha akiondoka kama mchezaji huru majira ya kiangazi.
Kuna tetesi
kuwa Chelsea na Manchester United wanamtaka nyota wa England, wakati ambapo Juventus
na Paris Saint-Germain wakiwa mbioni kumnasa.
David Villa, Barcelona.
Kama ilivyo
kwa Sneijder, Villa pia ni jina kubwa ambaye amekosa nafasi ya kikosi cha
kwanza katika klabu yake ya Barcelona lakini akionekana kuwa kivutio katika
klabu kubwa za ligi kuu ya England “Premier League”
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa katika kikosi kilicho anza cha Barcelona
katika michezo 6 tu kati ya michezo 17 ambayo Barcelona imecheza ya ligi kuu ya
Hispania ‘La Liga’ msimu huu ambapo sasa ameondoshwa rasmi katika orodha ya
wachezaji wa kikosi cha kwanza moja kwa moja.
Meneja wa Chelsea
Rafa Benitez inasemekana anataka kuwaunganisha wachezaji watatu wa timu ya
taifa ya Hispania,Villa,Fernando Torres na Juan Mata katika kikosi chake,
lakini Liverpool na Arsenal huenda wakaingia vitani kutaka saini yake. Pia
huenda El Guaje akasalia Camp Nou kupigania nafasi msimu huu na kusubiri
uhamisho wa majira ya kiangazi.
Marouane Fellaini, Everton
Nyota huyu
raia wa Belgian alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri msimu huu
katika ligi kuu ya soka nchini England ‘Premier League’ anasifika kwa kipaji,
akili na hata umbile la kisoka ikiwa ni pamoja na uwezo wa kumaliza mipira ya
mwisho akitoa msaada mkubwa katika sehemu ya kiungo ya Everton maarufu “Toffee”.
Fellaini alisaini
mkataba wa miaka mitano mwaka uliopita lakini inasemekana anataka kuondoka Goodison
Park, ambapo vilabu mbalimbali vikiwa vinataka huduma yake.
Real Madrid ni
moja kati ya klabu kubwa inayo muawania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25,
ambaye anasubiri kuona kama Everton itafuzu klabu bingwa Ulaya msimu huu na
kuamua hatma yake.
Mario Balotelli, Manchester City
Baada ya
kuwepo taarifa kwa muda mrefu kuwa huenda akaondoka katika klabu yake ya Manchester
City, Super Mario Balotelli huenda akatimiza azma hiyo hivi karibuni baada ya dirisha kufunguliwa.
Akiwa
amefunga goli moja msimu huu, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22
uwanjani ameonekana kutokuwa na thamani hususani kutokana na kuzongwa na matatizo
mengi ya nje ya uwanja.
Itategemea na
taarifa ipi utakayo amini juu ya habari za Balotteli lakini ukweli ni kwamba
meneja Roberto Mancini huenda akamuondosha kikosini ama akampa nafasi ya mwisho
kutegemeana na vile anaona inafa.
Kutokana pia
na City kuwa na azina kubwa ya washambuliaji, City huenda ikalazimika kukubali
taarifa za tetezi kwamba Milan ilikuwa ikimtaka kwa ada ya uhamisho ya pauni
milioni could be forced to accept a rumored 20.
Wilfried Zaha, Crystal Palace
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akivutia na kusisimua sana katika timu
inayoshiriki ligi ndogo ya pili kwa ukubwa nchini England(Championship) ya
Crystal Palace.
Ana mambo mengi yan kuvutia ikiwemo nguvu na
kipaji kiasi kupelekea kuitwa katika kikosi cha hivi karibuni cha timu ya taifa
England.
Zaha ameonyesha
wazi kutaka kuihama klabu yake mwezi januari ambapo tayari kuna klabu kama Liverpool,
Arsenal, Manchester United, Tottenham, Chelsea na hata Real Madrid zikiwa
zinamnyemelea na inaonekana wazi Palace haina ubavu wa kumzuia kiungo
waliomsajili kwa pauni milioni 15.
Benat Etxeberria, Real Betis
Kiungo huyu
ana umri wa miaka 25 raia wa hispania amekuwa anacheza soka la kupendeza katika
klabu ya Betis na kumekuwepo na taarifa za uwezekano mkubwa wa kuihama klabu yake
mwezi huu wa januari dirisha litakapo funguliw.
Kiungo huyo
wa zamani wa Bilbao hivi karibuni aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya
Hispania na kuna taarifa kuwa amekuwa akitakiwa na Barcelona.
Spartak
Moscow na Wolfsburg pia zimetajwa kumuhitaji kama ilivyo kwa vilabu vya England
ambavyo ni Tottenham, Liverpool Arsenal.
Bafetimbi Gomis, Lyon.
Nyota wa
kimataifa wa Ufaransa amekuwa katika kiwango kizuri katika msimu huu akiifungia
magoli 11 katika ligi kikosi cha Les Gones. Kwasasa klabu yake ya Lyon ya
nchini Ufaransa imefulia kiunchumi na inalazimika kumuuza mlinda mlango wake
nyota Hugo Lloris kwenda Tottenham majira ya kiangazi.
Gomis mwenye
umri wa miaka 27 huenda akajiunga na Chelsea na Liverpool ambao wote wako
mawindoni kumsaka mshambuliaji huyo aliyethaminishwa kwa pauni milioni 15.
No comments:
Post a Comment