Meneja wa Chelsea Rafa Benitez
anasema ana matumaini makubwa kuwa Chelsea itarejea katika mbio za kuwania taji
la ligi kuu ya nchin I England ‘Premier League’ baada ya mwaka mpya.
‘The Blues’ kwa
sasa wako nyuma ya vinara wa ligi hiyo Manchester United kwa alama 11 licha ya
kwamba wanamchezo mmoja mkononi ambao ulitokana na safari yao ya hivi karibuni
nchini Japan ambako walikuwa wakishiriki michuano ya kombe la dunia la vilabu.
Baada ya
ushindi wa kutakata wa mabao 8-0 dhidi ya Aston Villa jumapili iliyopita,
Chelsea sasa inajipanga na michezo mitatu dhidi ya Norwich, Everton na Queens
Park Rangers michezo ambayo itachezwa kabla ya januari 2, ambapo Benitez anaimani
timu kupitia michezo hiyo itafanikiwa kuwasogelea vinara Manchester United na
Manchester City walioko kileleni katika msimamo wa ligi.
Alipoulizwa kama
alishawahi kuwaambia wachezaji wake kuwa bado wanayo nafasi ya kutwaa taji
hilo, Benitezi amesema
"tutaliaona hilo baada ya
michezo miwili mpaka mitatu ijayo na utashuhudia hali ya kujiamini ikijengeka
miongoni mwao na hiyo ndio hatma ya yote”
"wana
tembea vizuri uwanjani, wanatengeneza nafasi sasa tunapaswa kuendeleza mwendo
huo na itakuwa rahisi kwangu kusema tunaweza kushindana".
Benitez
aliajiriwa kama meneja wa muda baada ya kufukuzwa kazi mtangilizi wake Roberto
Di Matteo mwezi November ambapo alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa
mashabiki wa klabu hiyo lakini alitulia na kuongeza nguvu kwa wachezaji wake
tangu alipowasili.
Juu ya hilo
amesema
"wachezaji
walikuwa makini tangu siku ya kwanza, walijua kuwa wanameneja mpya na
wanatakiwa kucheza soka na tangu siku hiyo walijitahidi kujifunza na kuongeza
juhudi na wamekuwa wakifanya hivyo"
Mlinzi wa Chelsea
Gary Cahill anaamini Benitez sasa ameanza kupata ushindi dhidi ya wapinzani
wake baada ya kuonyesha soka dhidi ya Aston Villa.
Yaya Toure ataka Man City kubadili mbinu kama si hivyo.....
Yaya Toure amesisitiza
kuwa Manchester City inapashwa kuwa ikibadilika mara kwa mara katika mbinu zake
za uchezaji kama wanataka kweli kulichukua tena taji la ligi kuu ya England
walilotwaa msimu uliopita.
Toure, ambaye
alikuwa msaada mkubwa katika harakati za kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza
baada ya miaka 44 kupita, anaamini wapinzani wao wanazijua mbinu zao na wanatumia
namna mbadala ya kutengua mbinu hizo za kiuchezaji
na kuharibu mapeni yao.
Kuelekea kwenye
mchezo wa leo ndani ya siku ya Boxing Day dhidi ya Sunderland, Toure anasisitiza
juu ya nia yake ya kumuona meneja Roberto Mancini ili kuangalia namna ya
kubadili mbinu kuendelea ushindi na kupata magoli zaidi.
Akiongea na
gazeti la the Sun amekaririwa akisema,
"msimu
huu tunashindwa kucheza ukilinganisha na msimu uliopota kwakuwa wapinzani wetu
wanajua jinsi tunavyocheza".
"wakati
meingine tunapaswa kubadilisha mfumo wetu ili kuzisimamisha hizi timu, timu
nyingine na wachezaji wao wanatambua jinsi tunavyocheza, wanatusoma na
wanafanyia kazi kutusimamisha. Hata zile timu zilizo chini katika msimamo wa
ligi wanatupa shida.
"timu
ambayo tuliifunga goli 4-0 msimu uliopita wamejifunza mfumo wetu wa uchezaji na
wamebadili mbinu ya kukabiliana na sisi. Hawataki kufungwa magoli mengi tena.
Kwasasa Manchester
City iko nyuma kwa alama nne kwa vinara Manchester United.
Rooney anasema kiwango kitarejea
katika mchezo dhid ya Toon
Baada ya
kuonekana kama vile sasa anakwisha na kufunikwa na Robie van Persie,
mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amesema moto wake utarejea kama kawida katika mchezo dhidi ya Newcastle
United.
Rooney hakufua
dafu jumapili katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kule Liberty
Stadium, ambapo hakuwa vizuri, akipoteza mipira mingi na kukosa magoli.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa England anasema mchezo wa sikukuu ya leo ni nafasi tosha
kurejesha heshima yake mbele ya mashabiki wake na wa United kwa ujumla akianza
na mchezo wa leo mbele ya wageni Newcastle katika dimba la Trafford.
Baada ya kugundua umri unamuacha, Del Piero ajitangazia mkataba mpya na klabu yake ya Sydney FC.
Alessandro
Del Piero amedokeza kuwa anatarajia kuongeza mkataba wake na klabu ya Sydney FC
inayocheza ligi kuu ya nchini Australia A-League
na kusema kuwa lengo lake katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka ni
kuhakikisha Sydney FC, inapanda katika usukani wa ligi hiyo.
Del Piero na
wachezaji wenzake wa timu hiyo wanahaha kuiondosha timu yao kutoka katika
nafasi ya chini ya msimamo wa ligi hiyo wakati huu ambapo wanaelekea katika
mchezo mgumu na wapinzani wao wakubwa wa jiji la Sydney Central Coast Mariners
mchezo utakaopigwa hapo kesho alhamisi.
Del Piero
mwenye umri wa miaka 38 bado hajafikia makubaliano na klabu yake ya kumuongezea
mkataba mwingine , lakini mwenyewe anaamini malengo yake ni kuendelea kusalia Sydney.
Licha ya uzee wake, Brad Friedel amaliza uvumi wa kuelekea Blackburn asaini tena na Tottenham.
Brad Friedel
amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Tottenham.
Mlinda mlango
huyo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika baada ya kumalizika
msimu huu wa ligi, tayari amesha kubaliana na klabu yake na kusaini mkataba mwingine
wa nyongeza wa mwaka mmoja kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka kiangazi 2014.
Friedel atakuwa
anakamilisha miaka 43 ya kuzaliwa kwake baada ya mkataba wa mpya kumalizika na anajipanga kuhakikisha anakuwa
mlinda mlango nambari moja wa klabu hiyo kama alivyokuwa akidhani kupata timu ya
kucheza kikosi cha kwanza baada ya mkataba wake kumalizika huko Hugo Lloris.
Spurs
imetangaza kumuongeza mkataba mlinda mlango huyo na kuwamaliza kabisa Blackburn
ambao walikuwa wakimtolea macho mkongwe huyo kwa lengo la kumrejesha Ewood
Park.
No comments:
Post a Comment