Lionel Messi akitoka neno la shukrani baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Baloon D'OR 2012. |
Mesi kulia akipiga picha ya pamoja na Cristiano Ronaldo kushoto na Andreas Iniesta katikati kabla ya kutangzwa mshindi. |
Kikosi cha wachezaji 11 bora wa mwaka 2012 (FIFA FIFPro World XI 2012). |
Washereheshaji walikuwa ni Ruud Gullit na Kay Murray. |
Mchezaji bora kwa upande wa wanawake Abby Wambach wa Marekaani akichukua tuzo yake baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo. |
Ronaldo wakati akiingia ukumbini. |
Mshambiliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel
Messi amevunja rekodi nyingine ya kukusanya tuzo ya nne ya mchezaji bora wa
shirikisho la soka duniani FIFA mfululizo katika kipindi cha miaka minne mfululizo tuzo inayotambulika kama ‘FIFA Ballon d’Or’, wakati
ambapo mmarekani Abby Wambach akipata tuzo hiyo kwa mara ya kwanza kwa upande wa wachezaji soka wanawake katika hafla iliyofanyika Zurich Kongresshaus usiku
huu.
Vicente del
Bosque, Kocha wa timu ya taifa ya Hispania na kocha wa timu ya taifa ya
wanawake ya Sweden, Pia Sundhage (ambaye pia ni kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani)
wakishinda tuzo hiyo kwa upande wa makocha wa timu za taifa.
Messi mwenye
umri wa miaka 25, aliukamilisha mwaka 2012 kwa kufunga jumla ya mabao 90. Sambamba na hilo pia aliibuka kuwa
mfungaji bora wa michuano ya vilabu ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kwa
msimu wa 2011-2012 baada ya kufunga jumla ya mabao 14.
Wakati hayo
yakiwa hivyo Vicente del Bosque ambaye alitwaa kombe la dunia kama kocha wa timu ya taifa ya Hispania mwaka 2010 na mwaka jana akatwaa taji lingine la mataifa ya Ulaya akiwa bado na Hispania yaani EURO 2012 ameshinda tuzo ya kocha bora.
Katika soka
la wanawake mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wa timu ya taifa ya Marekani ambapo Wambach ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka.
Sundhage na Wambach waliingoza Marekani kutwaa kwa mara ya pili medali ya dhahabu ya michezo ya Olympic jijini London baada ya kuichapa Japan katika mchezo wa fainali ikiwa ni kama kulipiza kisasi kufuatia Japan kuwachapa wamerekani hao huko nyuma ambapo Japan ilishinda kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo.
Sundhage na Wambach waliingoza Marekani kutwaa kwa mara ya pili medali ya dhahabu ya michezo ya Olympic jijini London baada ya kuichapa Japan katika mchezo wa fainali ikiwa ni kama kulipiza kisasi kufuatia Japan kuwachapa wamerekani hao huko nyuma ambapo Japan ilishinda kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo.
Tuzo hizo
zilkuwa ni matokeo ya kura ambazo zilipigwa na manahodha na makocha wa timu za
taifa za wanawake na wanaume pamoja wawakilishi waandishi wa habari
walioteuliwa na jarida la michezo la kifaransa la France Football, ambao
walipiga kura katika makundi yote manne ya waliopigiwa kura.
Kura katika kila kundi iliwakilisha robo ya matokeo ya mwisho.
Ulikuwa ni usiku ambao hautasahaulika ambao wachezaji wengi wa zamani na wasasa walijumuika katika zulia jekundu ‘Red carpet’.
Kura katika kila kundi iliwakilisha robo ya matokeo ya mwisho.
Ulikuwa ni usiku ambao hautasahaulika ambao wachezaji wengi wa zamani na wasasa walijumuika katika zulia jekundu ‘Red carpet’.
Waliohudhuria waliburudika na ladha za burudani mbalimbali kutoka nchini Brazil wakati huu ambapo huu ambapo tunaelekea katika michuano ya kombe la shirikisho mwaka huu 2013, pamoja na burudani ya muziki kutoka kwa mwanamuziki kutoka nchini Scotland Amy MacDonald.
Lionel Messi
ameshinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or baada ya kupata asilimia 41.60% ya kura zote
akiwa mbele ya Cristiano Ronaldo aliyepata asilimia 23.68% na Andrés Iniesta akipata
asilimia 10.91% ya kura zote.
Wambach, mshindi
wa tuzo kwa upande wa wanawake aliingoza Marekani nchini Uingereza katika
michuano ya Olympics 2012 jijini London, ambako huko alishinda tuzo ya mpira wa
dhahabu ya kampuni ya Adidas ‘adidas Golden Ball’ kama mchezaji bora wa
mashindano na pia tuzo ya ufungaji bora ya Adidas (adidas Golden Boot) baada ya
kupachika wavuni jumla ya magoli 5.
Amepata asilimia
20.67% ya kura zotr akiwashinda Mbrazil Marta na Alex Morgan kutoka Marekani
ambao walipata asilimia 13.50% na 10.87% ya kura zote zilizopigwa.
Vicente del
Bosque kama kocha bora wa timu ya za wanaume wa FIFA amepata asilimia 34.51% ya
kura zote akiwashinda José Mourinho, kocha wa Ureno na klabu ya Real Madrid, aliyepata
asilimia 20.49%, na kocha wa zamani wa FC Barcelona Pep Guardiola, aliyepata asilimia
12.91% ya kura zilizopigwa.
Wakati hayo
yakiwa hivyo naye Pia Sundhage amekuwa kocha wa timu za wanawake wa mwaka baada
ya kukusanya asilimia 28.59% ya kura zote akiwashinda Norio Sasaki wa Japan aliyepata
asilimia 23.83% aliyefanikiwa kupata
medali ya fedha katika michezo ya Olympics jijini London, na kocha wa timu ya
taifa ya Ufaransa Bruno Bini aliyepata asilimia 9.02%.
FIFPro, muungano
wa wachezaji wa duniani iliwaalika jumla ya wachezaji wakulipwa 50,000 kutoka
sehemu mbalimbali duniani kuchagua timu bora ya mwaka 2012 (FIFA FIFPro World
XI 2012).
Waliochaguliwa
ni pamoja na
Mlinda mlango -Iker Casillas (Spain)
Walinzi -Dani Alves (Brazil), Marcelo (Brazil), Gerard Piqué (Spain) na Sergio
Ramos (Spain)
Viungo-Xabi
Alonso (Spain), Andrés Iniesta (Spain) na Xavi Hernández (Spain)
Washambuliaji- Cristiano Ronaldo
(Portugal), Radamel Falcao (Colombia) na Lionel Messi (Argentina).
Tuzo
nyingine maarufu ilikuwa ni ‘FIFA Puskás Award’ ambayo inatoka kwa goli bora la
mwaka ambayo inapigiwa kura kupitia mtandao wa FIFA ambapo goli hilo linawekwa
katika mtandao wa FIFA.com kupitia YouTube na mtandao mwingine wa ‘francefootball.fr’
ambapo mashabiki zaidi ya milioni 5 wanawakilisha katika kulipigia kura goli
hilo.
Tuzo hiyo
kwa mara ya kwanza ilizinduliwa 2009 kwa heshima ya nyota na nahodha wa zamani
wa Hungary Ferenc Puskás, ambaye alikuwa nahodha wa Hungary miaka ya 1950.
Kwa mara ya
kwanza tuzo hiyo ilichukuliwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Slovakia Miroslav
Stoch, ambaye alifunga goli katika kisambusa cha ndani ya nyavu hiyo ilikuwa
tarehe 3 March 2012 akiwa na klabu yake ya Fenerbahçe katika ligi kuu ya nchini
Uturuki dhidi ya Gençlerbirliği.
Franz
Beckenbauer amepewa tuzo ya heshima ya Rais wa FIFA Joseph S. Blatter katika
kutambua mafanikio yake na rikodi yake nzuri katika soka kama mchezaji wa zamani lakini pia kama mshauri.
Tuzo ya FIFA
ya mchezo wa kiungwana ‘FIFA Fair Play Award ‘ imekwenda kwa shirikisho la soka
la Uzbekistan (UFF).
No comments:
Post a Comment