KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, February 13, 2013

HUKUMU YA MAKATI YA RUFAA YA UCHAGUZI YA TFF, JAMALI MALINZI ANASUBIRI HEKIMA ZA

 




JAMALI MALINZI
SLP 10000 DAR ES SALAAM
13/FEBRUARI/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH:KUENGULIWA KWANGU KUGOMBEA URAIS WA TFF 2013
Ndugu zangu, kupitia vyombo vyenu vya habari ninaomba nieleze umma wa watanzania hususani wadau wa mpira wa miguu yafuatayo kuhusu kuenguliwa kwangu.
Awali ya yote nieleze kusikitishwa kwangu na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya rufaa ya TFF ya kuniengua kugombea urai s wa TFF.Sikubaliani na maamuzi yaha.
Katika kuniengua kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF imetoa sababu mbili (nanukuu magazeti ya jana tarehe 12/02/2013 maana hadi leo sijakabidhiwa barua ya kuenguliwa)
1.Kukosa uadilifu kwa kupinga waraka uliotolewa na TFF wa kubadili katiba ya TFF mwezi Desemba 2012.
2.Kukosa uzoefu wa miaka mitano ya uongozi.
Ndugu zangu kiini cha maamuzi ya kamati ya rufaa dhidi yangu ni pingamizi lililowekwa na mtu mmoja anayeitwa AGAPE FUE. Bwana Agape Fue aliniwekea pingamizi katika kamati ya uchaguzi akidai mimi nilipinga waraka wa kubadili katiba ya TFF na pia sina uzoefu uzoefu wa mika mitano ya uongozi wa mpira. Kinyume na matakwa ya kamati ya uchaguzi kama yalivyotangazwa kuwa mtoa pingamizi aje mwenyewe kutetea pingamizi lake , bwana Agape Fue hakutokea mbele ya kamati ya bwana Lyato. Matokeo yake tarehe 31/01/2012 kamati ya uchaguzi ya TFF ilitoa maamuzi ya kutupilia mbali pingamizi hilo.
Bwana Agape Fue hakuishia hapo kwa mara nyingine tarehe 06/02/2013 alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi akidai kamati ya uchaguzi haikumtendea haki. Rufaa hii haikuwa na anwani wala namba ya simu ya Bw Agape Fue ilisikilizwa tarehe 10/02/2013 na maamuzi ya kukata jina langu yakatangazwa jioni ya tarehe 11/02/2013.
Mpaka leo najiuliza hivi huyu Bw Agape Fue ni mwanaume au ni mwanamke? (hakueleza kama ni Bwana au Bibi Agape Fue). Agape Fue ni nani hasa? Anaishi wapi? Je ni Mtanzania au sio Mtanzania maana kikanuni wasio watanzania hawaruhusiwi kujihusisha na uchaguzi wa TFF (rejea kifungu cha 9 cha kanuni za uchaguzi),pingamizi lake halikuambatana na udhibititisho wa uraia. Kwa nini alichukua maamuzi haya? Sipata jibu. Iweje achukue maamuzi mazito ya kumkatia mtu rufaa kisha uishie kusaini karatasi na kwaachia wengine wakusemee na usije hata kushuhudia kinachoendelea kama kweli una maslahi na madai yako? Waandishi wa habari mnisaidie kupata majibu.


Ndugu zangu, mtoa pingamizi alidai haikuwa sahihi kupinga azimiao la kubadili katiba ya TFF kwa njia ya waraja . Naomba nisisitize mambo matatu:
1.       Wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wanawakilisha matakwa ya vyama vilivyowatuma kwenda kwenye mkutano mkuu wa TFF, na ndio ndio maana chama cha mpira cha mkoa wa Kagera(KRFA) kiliitisha kikao cha kamati ya utendaji ili kamati iweze kutoa mwongozo kwa wajumbe wake kuhusu nini kifanyike kuhusu waraka ulioletwa na TFF, hivyo maamuzi ya yaliyotolewa ya kuukataa waraka huo yalikuwa ni maamuzi ya chama cha mpira mkoa wa Kagerana wala haya kuwa maamuzi maamuzi ya Jamali Malinzi, iweje Malinzi niadhibiwe kwa maamuzi haya, kwani nini usiadhibiwe mkoa mzima na mikoa yote iliyopinga waraka? Hii ni haki kweli? Siamini kama kuna mjumbe wa mkutano mkuu aliyekiuka maamuzi ya kamati yake ya utendaji.
2.       Katika mchakato wa kubadili katiba kwa njia ya waraka kilichokuwa kinagomba sio maudhui (content) ya mabadiliko ya katiba bali utaratibu uliotumika kubadili katiba. Swali la msingi tulilojiuliza ni wajumbe wa kamati ya utendaji KRFA ni kwamba je kwa mujiibu wa katiba ya TFF kifungu 22 na kifungu 30 wapi katiba inatamka kuwa inaweza kubadilishwa kwa njia ya waraka? Mpaka leo hilo jibu hakuna , labda aliyeniwekea pingamizi atusaidie kupata jibu la swali hili. Katiba ya TFF iko wazi kabisa inatamka kuwa katiba itabadilishwa kwa njia ya mkutano mkuu tu( General assembly).
3.        Ni kweli FIFA iliagiza yafanyike mabadiliko ya katiba ya kuingiza kipengele cha ‘club licencing’ katika katiba , lakini je FIFA katika agizo hilo ilisema katiba ya ya TFF ivunjwe ili kutimiza azma hiyo? Ikimbukwe kuwa mwaka 2004 FIFA iliagiza TFF aiingize kwenye katiba kipengele cha katibu mkuu awe wa kuajriwa badala ya kuchaguliwa, agizo lilitekelezwa kwa kupitishwa na mkutano mkuu wa TFF, iweje leo utaratibu huu ukiukwe? Hata majuzi CAF walipotaka kubadili katiba ili Rais wa CAF atokane na wajumbe wa kamati ya utendaji jambo hili lilitekelezwa kwa kuitisha mkutano mkuu wa dharura uliofanyika Seychelles majuzi. Katiba ndio msingi  mkuu wa uendeshaji  wa TFF, nitaipigania siku zote. Huu ndio utaratibu , si CAF si  FIFA si vyama vyama vya mpira vya nchi, hakuna anayebadili katiba kwa njia ya waraka, kama kuna mwenye ushahidi aulete.
Kuenguliwa jina langu eti kwa kuwa nilipinga waraka wa kubadili katiba sio uamuzi sahihi.
Kuhusu uzoefu wa miaka mitano katika uongozi:
Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa TFF mwaka 2008 niligombea na jina langu lilikatwa na kamati ya uchaguzi ya TFF.  Nilikata rufaa katika kamati ya rufaa ya TFF na kushinda . Hukumu hii ni halali hadi leo . Iweje leo miaka minne baadaye kamati hiyo hiyo ya rufaa ( kubadili kubadili majina ya wajumbe sio kubadili taasisi) inione sina uzoefu? Si hilo tu, hata katika kujaza fomu namba moja ya kugombea niliambatanisha vielelezo vyote vya uzoefu wangu ikiwa ni pamoja na kudhibitisha kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita nimekuwa :
-Mjumbe wa Baraza la michezo mkoa wa Dar es Salaam.
-Mwenyekiti wa kamati ya mashindano chama cha mpira mkoa wa Pwani COREFA.
-Mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Kagera.
-Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Kagera.
Hii ni pamoja na kuongoza Yanga 2002 -2005
Hivi katika nafasi hizi za uongozi ipi ni ya kuongoza ‘Bonanza’? Nimedhalilishwa sana.

HITIMISHO.
Vyombo vya habari kupitia nakala, tahariri na maoni ya wasikilizaji /wasomaji/watazamaji vimesifia sana awamu mbili za uongozi wa Bwana Tenga. Bwana Tenga amesifiwa kwa umahiri wake wa kuleta utulivu katika sekta ya mpira wa miguu Tanzania. Amesifiwa kwa kujenga taasisi imara ambayo mhimili wake mkuu ni sekretarieti makini na kamati mbaloimbali zilizo imara. Let him rise to the occasion, muda wa kuonyesha uongozi imara ni huu, historia itamhukumu kwa jinsi gani atasimamia suala hili , haki sio lazima itendekea lakini pia inatakiwa ionekane inatendekea.
Kamati ya utendaji ya TFF inayo mamlaka ya kubatilisha maamuzi haya kwa maslahi ya mpira wa Tanzania. Ninamshauri Rais wa TFF aitishe kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ili kijadili hali hii na kunirudishia haki yangu ya kugombea urais wa TFF.
Nihitimishe kwa kuwaomba wadau wa mpira wa miguu Tanzania wawe watulivu wakati tukisubiri kupata ufumbuzi wa suala hili

Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania.
Ahsanteni sana.
Jamali Emil Malinzi
Dar es Salaam
13/02/2013

No comments:

Post a Comment