Shangwe
na furaha: wachezaji wa Nigeria wakinyanyua juu kombe la ubingwa ikiwa
ni mara ya tatu kulinyakua katika historia ya fainali hizo.
|
Nigeria imefanikiwa kuchukua kwa mara ya tatu taji la soka la mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Bukina Faso bao 1-0 huku Nigeria ikitawala mchezo wa fainali uliopigwa jijini Johannesburg.
Sunday
Mba aliifungia Nigeria maarufu kama 'Super Eagles' bao hilo zuri kwa mpira wa kubetua na kuusukumiza wavuni mpira wa kunyunyiza 'volley' zikiwa zimesalia dakika tano kabla ya mapumziko baada ya muda mrefu wa kutafutana kwa tahadhari kubwa, huku pongezi kubwa zikimuangukia kocha mzalendo na nahodha wa zamani wa timu hiyo Stephen Keshi.
Sunday Mba akijaribu kuubetua mpira juu ya mlinzi wa Bukina Faso kabla ya kuusukumiza wavuni na kuwa goli pekee lililo ipa ushindi Nigeria. Picha ya chini Mba na wachezaji wengine wa Nigeria wakishangilia baada ya goli kuingia.
Hiyo ilikuwa ni fainali ya kwanza kwa Nigeria tangu mwaka 2000 lakini pia walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo tangu mapema kufuatia rikodi yao ya kucheza michezo 12 bila ya kufungwa.
Vincent Enyeama akipaa angani kuunyakuwa mpira licha ya kukabiliwa na Prejuce Nakoulma.
Baada ya Nigeria kufanikiwa kutwaa taji hilo, mantiki yake ni kuwa kocha Keshi anakuwa kocha wa pili kushinda taji hilo akiwa mchezaji na pia kama kocha akifuata nyayo za Mahmoud Al Gohari wa Misri.
Mlinda mlango wa Nigeria Vinvent Enyeama akikabiliana na Mady Panandetiguiri.
Victor Moses wa Nigeria akijaribu kuuwahi mpira huku akipata upinzani kutoka kwa Bakary Kone wa Bukina Faso(katikati), Mohamed Koffi
(nyuma) na Djakaridja Kone (kulia).
Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Burkina Faso
kufikia fainali ya michuano hiyo ambapo mwaka 1998 walifanikiwa kutinga hatua ya nufu fainali ambapo walipoteza mchezo huo kwa waliokuwa mabingwa Misri.
Pamoja na kufungwa lakini walionyesha uwezo ambapo katika sehemu ya kiungo Jonathan Pitroipa alionyesha ubunifu mkubwa na kutawala sehemu hiyo.
Itakumbukwa Pitroipa ndiye aliyepewa kadi nyekundu kimakosa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ghana.
Mlinda mlango wa Burkina Faso Daouda Diakite akizuia hatari kutoka kwa washambuliaji wa Nigeria.
Rais wa FIFA Sepp Blatter alikuwepo uwanjani.
No comments:
Post a Comment