Timu ya taifa ya Mali imefanikiwa kumaliza michuano ya mataifa ya Afrika kwa kushika mnafasi ya 3 kufuatia kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ghana.
Mahamadou Samassa aliipa bao la uongozi Mali kwa kufunga bao la kichwa cha kuchumpa kabla ya nahodha Seydou Keita kuandika bao la pili baada ya kupokea mpira wa krosi na kuuzamisha pembveni kabisa mwa mlinda mlango wa Ghana.
Ghana ilikosa penati ilipigwa na Mubarak
Wakaso kabla ya kuandika bao Kwadwo Asamoah.
Mali alifanikiwa kukandamiza msumari wa mwisho katika dakika za majeruhi kupitia kwa Sigamary Diarra wakati Ghana wakisaka bao la kusawazisha.
Hii ni mara ya pili Mali inailambisha mchanga Ghana katika mchezo wa kusaka nafasi ya tatu katika michuano ya AFCON, ilifanya hivyo mwaka jana 2012
No comments:
Post a Comment