Jack Wilshere aligumia maumivu wakati akipatiwa matibabu baada ya kugongana na Alfred N'Diaye.
|
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere
amelazimika kutolewa uwanjani katika dakika za mwisho za mchezo wao dhidi ya Sunderland mchezo ambao umemalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Jack Wilshere amepatwa namaumivu ya paja baada ya kukabilianana Alfred N'Diaye.
Haikuwa ni dhoruba kubwa kati yake na nyota huyo mpya wa Sunderland, lakini Wilshere alilazimika kuondolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Abou Diaby ambapo ilikuwa ikitaka kulinda ushindi katika mchezo wa leo.
Arsene Wenger alionekana kukasirishwa na aina ya tackling aliyofanyiwa kiungo wake ambapo inavyoonekana ni wazi kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mchezo mmoja.
Meneja huyo wa Arsenal baada ya mchezo amesikika akisema anamatumaini kuwa Wilsheakuwa njen ya uwanja kwa siku chache jambo ambalo limeonekana kuleta nafuu ya hofu yake.
Katika mchezo huo uliopigwa Stadium of Light, bao la Arsenal lilifungwa na Santi Cazorla katika kipindi cha kwanza kwa shuti la chini chini na kumpita mlinda mlango Simon Mignolet.
Wilshere na N'Diaye katika vita ya kuwania mpira.
Titus Bramble akifanya tackling kwa kiungo wa Arsenal.
Wilshere na Lee Cattermole wakionyeshana uwezo katika eneo la kiungo.
Shambulizi la Santi Cazorla lillilozaa goli la mchezo.
No comments:
Post a Comment