Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena hii leo kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja vinne tofauti hapa nchini
Katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wenyeji Kagera sugar walikuwa dimbani wakicheza dhidi ya Mgambo Shooting mchezo ambao wenyeji wameibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mchezo mwingine ulikuwa ni katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Toto Afrika waliwakaribisha Coast Union ya Tanga na matokeo ni ya mchezo huo kwamba timu hizo zimekwenda sare ya 0-0.
Kule karika dimba la Sokoine mkoni Mbeya wenyeji Tanzania Prisons walikuwa wenyeji wa Afrikan Lyon ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo katika mchezo huo wenyeji wamefanikiwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumba kufuatia kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Mchezo mwingine uliochezwa hii leo ni kule mkoani Arusha katika dimba la Sheikh Amri Abeid Kaluta ambapo wenyeji JKT Oljoro walikuwa wenyeji wa bingwa mtetezi wa taji la ligi kuu Simba, mchezo ambao umamalizika kwa Simba kushikwa shati na kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Simba ilianza kupata bao katika za mapema za kuanza mchezo kupitia kwa kiungo Mwinyi Kazimoto huku wenyeji Oljoro wakifanikiwa kusawazisha katika kipindi cha pili kupitia kwa Paul Nonga.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha jumla ya alama 28 na kusalia katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, ilhali Coast Union baada ya sare yao ya leo nao wakifikisha alama 27.
Tanzania Prisons baada ya ushindi wa leo wamefikisha alama 18.
Kagera Sugar baada ya kuichapa Mgambo ya Tanga wamefikisha alama 24 sawa na Ruvu Shooting ambao hii hawakushuka uwanjani.
Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho ambapo Mtibwa Sugar watakuwa wakiwakaribisha Azam fc kutoka jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment