Ruud van Nistelrooy anaamini viwango vya sasa vya wachezaji Robin van Persie na Cristiano Ronaldo vitakuwa ndio chachu ya maamuzi ya ushindi wa mchezo wa hatua ya mtoano wa 16 bora wa vilabu bingwa barani Ulaya baina ya vilabu vyake vya zamani vya Manchester United na Real Madrid.
Van
Nistelrooyano aliitumikia United kwa miaka mitano kabla ya kuelekea Madrid mwaka 2006 ambako aliitumikia kwa miaka minne katika viunga vya Bernabeu, anadhani kuwa ni vigumu kujua ni timu gani kali kati ya hizo mbili itakayo ibuka na ushindi.
Ruud van Nistelrooy anaadhani mpiga mabao wa United, Van Persie na mpiga mabao wa Madrid ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa United, Ronaldo ndio wa kura ya timu gani itaibuka na ushindi jumatano.
'kwa upande wangu utofauti utaletwa na viwango vya uchezaji vya Cristiano na Van Persie. Nadhani mmoja kati ya wachezaji hao ataleta utofauti wa matokeo ya mchezo,'
'Timu zote zinafanya vizuri. Nadhani Madrid imeimarika kwa kiasi kikubwa katika wiki za hivi karibuni, achilia mbali matokeo ya mchezo dhidi ya Granada ambapo walifungwa goli 1-0. Naiona ni timu ngumu, ambayo ilicheza vizuri dhidi ya Barca na wanaonyesha ubora wao katika michezo migumu.
'Nadhani mtanange huo utaamuliwa na vitu vidogo.'
Ruud van Nistelrooy aliihama Manchester United na kujiunga na Real Madrid mwaka 2006.
Wayne Rooney, ambaye alifunga goli la England wiki hii amerejea katika kasi yake.
Mduchi Ruud van Nistelrooy mwenye umri wa miaka 36 anadhani Madrid ambayo inasaka rekodi ya kushinda taji la Ulaya kwa mara ya 10 imeimarika zaidi kiubora kuliko kikosi cha Sir Alex Ferguson lakini ameionya Madrid kuwa makini na uwezo wa safu ya ushambuliaji ya United ambayo ina washambuliaji wenye uchu wa magoli kama Van Persie na Wayne Rooney.
'Madrid kutokana na kukabiliwa na majeruhi haijaweza kuunga kikosi imara na kupata kikosi kimoja kilicho imara kila wiki.
'Pepe
na Marcelo wamekuwa majeruhi, Gonzalo Higuain na Karim Benzema
hawako vizuri, Angel Di Maria hachezi mara kwa mara, pamoja na majeruhi kwa mlinda mlango Iker Casillas.
Ronaldo amekuwa mfungaji wa Real Madrid tangu ajiunge nayo kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 82 akitokea Manchester United.
Sir Alex Ferguson na Roberto Mancini wanaamini Van Persie amekuwa jembe la kuipeleka United kileleni.
Ronaldo atakuwa akicheza dhidi ya timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu aondoke 2009.
No comments:
Post a Comment