KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 9, 2013

Everton kumkosa Tim Howard kwa wiki nne na Licha ya kuonekana na kumbwela msimu, wakala wa Samir Nasri anasema ataendelea kumpigania city..


Mlinda mlango wa Everton Tim Howard atalazimika kuwa pembeni ya uwanja kutokana na kuthibika kuwa mlinda huyo amevunjika mfupa wa mgongo.
Mlinda mlango huyo raia wa marekani mwenye umri wa miaka 34 amepatwa na dhahma hiyo katika mchezo wa marudiano wa michuano ya FA  mzunguko wa tano dhidi ya Oldham siku 11 ziliaopita
Meneja wake David Moyes anadhani  Howard huenda akaendelea kuwepo nje ya uwanja kwa wiki nne.
Mlinda mlango wa kimataifa wa Slovakia Jan Mucha, ambaye alianza kuichezea timu hiyo wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Reading, ataendelea kuwepo katika goli la timu hiyo katika mchezo wa robo fainali ya dhidi ya Wigan hii leo.

Licha ya kumbwela msimu, wakala wa Samir Nasri  anasema ataendelea kumpigania city.



Wakala wa Samir Nasri  amesisitiza kuwa atahakikisha anapigania hatma ya baadaye ya nyota ndani ya Manchester City.
Nyota huyo wa kimataifa wa ufaransa mwenye umri wa miaka  25 amekuwa mbali na mafanikio yake msimu huu akiwa pia ameanza katika kikosi cha kwanza nusu tu ya michezo ya ligi ya  Manchester City
Nasri amekuwa akikosolewa waziwazi na meneja wake Roberto Mancini kutoka na kiwango chake cha msimu huu, hali ambayo imekuja baada ya kampeni ngumu ya Euro 2012 ambapo Nasri alizozana na mwandishi wa habari na kupelekea kufungiwa na michezo mitatu na shirikisho la soka la nchi yake ya Ufaransa FFF.
Licha ya yote hayo kumkumba Nasri, bado wakala wake Jean-Pierre Bernes anadhani mshambuliaji huyo atarejea katika hali yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment