KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, April 10, 2013

KIMATAIFA : Watakao bagua kwa rangi Ulaya kufungiwa michezo kumi, Equatorial guinea huenda ikapoteza ushindi wao dhidi ya cepe verde na RAFA BERNITEZ: GARY CAHILL AFANYIWA UPASUAJI.

Shirikisho la soka barani Ulaya EUFA limesema limegundua kujitokeza kwa vitendo vya kibaguzi kwa baadhi ya wachezaji na maafisa kadhaa sasa huneda wakakabiliwa na kifungo cha michezo 10 ikiwa ni sehemu ya mpango mpya uliopendekezwa na EUFA.
 Katibu mkuu wa shirikisho hilo Gianni Infantino amesema vilabu vitakavyogundulika na tuhuma hizo huenda vikalazimika kufunga sehemu ya uwanja wao ambazo mashabiki wao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo.

Kumekuwepo na gumzo kubwa juu ya vitendo vya aina hiyo ambavyo vimekuwa vikijitokeza msimu huu hususani baada ya kiungo wa AC Milan Kevin-Prince Boateng kuongoza baadhi wa wachezaji wenzake kutoka uwanjani katika mchezo mmoja wa kirafiki nchini Italia.

Raia huyo wa Ghana aliondoka uwanjani katika mchezo dhidi ya Pro Patria baada ya kusikika maneno ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki.

Akiongea katika mkutano wa Soccerex Global Convention 2013 jijini Manchester hii leo Infantino amesema kuwa mkutano huo ni mkubwa wa kibiashara katika soka ambaopo amenukuliwa akisema.
 "Ina maana kuwa sehemu ambayo itapatikana na hatia ya kurusha maneno ya kibaguzi itafungwa pamoja kupigwa faini ya euro 50,000 (£42,700)"

Huko nyuma nahodha wa Chelsea John Terry na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez waliiingia matatizoni baada ya kukumbana na kashfa ya kutumia lugha za kibaguzi.

Mwezi Mei kamati ya utendaji ya Uefa inatarajiwa kupigia kura mapendekezo hayo jijini London na huenda sheria hiyo ikaanza kutumika katika michuano ya Uefa kuanzia mapema mwezi Julai.

Mkutano wa November  23 mpaka 27/ 2013 utakuwa unakamilisha sehemu ya mwisho ya mkutano wa Soccerex Global Convention ambao utafanyika Rio de Janeiro.

Mkutano huu ni flagship ambayo inakutanisha maamuzi makubwa ya kisoka ambapo zaidi ya wajumbe 4,500 wanakutana kwa siku tano za kufahamina, kujifunza na kuzungumza biashara.

Mkutano wa Rio utakuwa unaweka mipango ya miaka minne ijayo katika eneo la maendeleo ya biashara ya soka, kabla ya kombe la dunia la FIFA 2014 na michuanio ya Olympic 2016 kabla ya kuangalia fursa mbalimbali kuelekea michuano hiyo mikubwa.

Equatorial guinea huenda ikapoteza ushindi wao dhidi ya cepe verde
Timu ya taifa ya Equitorial Guinea kufungiwa kwa kutumia wachezaji si wazawa.
 Equatorial Guinea huenda ikavuliwa ushindi wao wa bao 4-3 dhidi ya Cape Verde mchezo wa kufuzu kombe la dunia 2014, kufuatia kumchezesha mchezaji ambaye hakuwa halali kutumiwa na timu hiyo.

Fifa imesema imefungua kesi dhidi ya chama cha soka cha Equatorial Guinea FA baada ya ushindi wao wa mwezi uliopita uliofanyika mjini Malabo kufuatia kutuhumiwa na Cape Verde.

Bodi ya utawala ya FIFA imesema bado haijathibitisha juu ya tuhuma hizo na kwamba bado wanaendelea na uchunguzi.

Kwa mujibu wa kifungu nambari cha 17 cha katiba ya FIFA kinasema kuwa ili mchezaji kuwa halali kutumikia timu ya taifa anapaswa kuwa mzaliwa wa taifa husika ambapo mmoja wa wazazi wake anapaswa kuwa rai wa taifa hilo.

Kifungu hicho pia kinasema kuwa mchezaji anaweza kuwa halali endapo kati ya babu au bibi alizaliwa katika taifa husika .

Mataifa ya Burkina Faso , Gabon na Sudan tayari yamekutana na matatizo ya aina hiyo katika michezo yao ya kuwania kufuzu kombe la dunia 2014.

Equatorial Guinea kwasasa iko katika nafasi ya tatu katika kundi B wakiwa na alama tano huku kundi hilo likiongozwa na Tunisia ambao wameshinda michezo yote mitatu ya kundi hilo na wakiwa na alama 9.

 RAFA BERNITEZ: GARY CAHILL AFANYIWA UPASUAJI
MenejaChelsea Rafa Benitez amethibtisha kuwa mchezaji wake Gary Cahill amefanyiwa upasuaji wa mguu.
Cahil ambaye ana umri wa miaka 27 alienguliwa kutoka katika kikosi cha timu ya taifa ya England maarufu kama Simba watatu kilichokuwa katika kampeni ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino na Montenegro, lakini pia alikuwa nje katika wa mchezo wa ligi baina ya Chelsea dhidi ya West Ham March 17.
Cahill pia hakusafiri kuelekea nchini Russia kwenye mchezo wa pili wa michuano ya Europa League hatua ya robo dhidi ya Rubin Kazan ambapo pia anatarajiwa  kutokuwepo uwanjani katika kipindi kisichopungua wiki mbili.

Amekaririwa Benitez akisema 
"Tulifanya hilo kwa haraka siku ya Jumamosi wakati wa mchezo dhidi ya Southampton Machi 30"

Mlinzi huyo wa kati wa Aston Villa na Bolton ameitumikia klabu yake jumla ya michezo 24 ya Premier League msimu huu ambapo Benitez anadhani atafanikiwa kuponya tatizo lake kwa haraka ambapo wakati huu atakuwa akimtegemea mlinzi mwingine Ryan Bertrand .

No comments:

Post a Comment