KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, May 25, 2013

INTER MILAN YAMTANGAZA MENEJA WA NAPOLI WALTER MAZZARRI KUWA MRITHI WA STRAMACCIONI.

Walter Mazzarri meneja mpya wa Inter Milan.

Inter Milan imemtangaza meneja wa zamani wa Napoli Walter Mazzarri kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Bosi wa zamani wa Inter Andrea Stramaccioni mwenye umri wa miaka 37, alifukuzwa kazi kufuatia kufungwa michezo minne mfululizo katika jumla ya michezo mitano na kupelekea kumaliza katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi iliyomaliza ya Serie A.

Mazzarri mwenye umri wa miaka 51 aliondoka Napoli  Jumapili baada ya misimu minne ya kuiongoza klabu hiyo na kumaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
 
Taarifa ya Inter Milan imesema 
"FC Internazionale ingependa kumshukuru Andrea Stramaccioni kwa kazi yake kubwa aliyoinyesha hususani katika mwaka mgumu." 

Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amekanusha taarifa ya kwamba amemchukua Rafel Bernitez kuchukua nafasi ya Mazzarri.
 
Benitez mwenye umri wa miaka 53, kwasasa anatafuta kazi baada ya kumaliza muda wake wa kuifundisha Chelsea kwa muda ambapo ameipa mafanikio ya kutwaa taji la Ulaya la Europa league na kumaliza katika nafasi ya tatu katika ligi kuu ya soka ya England.

No comments:

Post a Comment