Kuelekea
mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young
Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17
zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya
Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo
huo.
Akiongea na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao
makuu ya klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali
(Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yangaa kitaibuka na ushindi
katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17
na kanuni za soka.
Akilimali amesema Yanga ni timu bora kwa sasa
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna
wachezaji wazuri wenye kiwango cha hali ya juu ambao wamepikwa
wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao ndio yaliyotupatia ubingwa
kabla ya ligi kumalizika.
Aidha aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba
tutamfunga Simba SC siku ya mei 18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na
uongozi bora chini ya mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement
Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda
wote huuu".
Naye Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi
ushindi katika mchezo huo, idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa
tunasema lazima tumfunge Simba mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe
kwa kufuata kanuni 17, na kama wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae
kupokea mvua ya mawe siku hiyo.
"Mwaka jana walitufunga kwa sababu
hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja
kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa
kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema mzee
Mwika.
TAMKO
RASMI LA WAZEE WA YANGA
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wazee wa YANGA, Napenda
Kuwafahamisha kuwa Wazee wa YANGA wamefurahi na kuwashukuru Viongozi wa Klabu
ya YANGA chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga kwa
kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa
mwaka 2012/2013. Ushindi huu umetokana na Uongozi bora, uwajibikaji katika
kutekeleza majukumu ya Klabu na kufikia malengo.
Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani
ya Uongozi, wanachama na wachezaji wetu.
Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na
viongozi na wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013
kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha,
shangwe na nderemo.
“YANGA
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
K.n.y: YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na MWENYEKITI WA WAZEE YANGA
ALHAJ JABIRI M. KATUNDU
Naomba kuwasilisha.
IBRAHIM
O. AKILIMALI
KATIBU
WA WAZEE WA YANGA
No comments:
Post a Comment