Kiungo wa Manchester City Yaya Toure amesema kuwa yuko fiti kuweza kuwakabilia Wigan jumamosi katika mchezo wa fainali ya michuano ya FA.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Caost alicheza dakika 45 tu katika mchezo wa ligi kuu ya England jumamosi iliyopita ambao walikwenda sare na Swansea huku taarifa zikiarifu kuwa alikuwa katika hali ya mchoko ambapo pia katika mchezo dhidi ya West Brom alilazimika kuwekwa benchi.
Akikaririwa amesema
"Wakatia mwingine kucheza katika kiwango kile kile na unalazimika kuepuka majeraha,"
said the 29-year-old.
City itakuwa ikitaka kupata taji katika msimu huu baada ya kupoteza taji la ligi kuu kwa Manchester United na pia ilifanya vibaya katika Champions
League baada ya kushika nafasi mwisho katika kundi.
Toure ambaye amefunga jumla ya mabao 11 msimu huu amekuwa msaada mkubwa katika kuhakikisha City inapata nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya Ulaya wakisubiri fainali ya Europe katika dimba la Wembley.
No comments:
Post a Comment