Orodha ya viwango vya ubora wa soka vilivyotolewa leo na shirikisho la soka duniani FIFA vimeonyesha kuwa Tanzania imesalia katika nafasi yake ya 33 barani Afrika huku wakiendelea kushika nafasi ya 116 duniani huku Ivory Coast wakiongoza Afrika na kushika nafasi ya 12 duniani.
Katika orodha hiyo Hispania inaendelea kuongoza ikiwa ikifuatiwa na Ujerumani huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na tatu ikikamatwa na Agentina.
Croatia wanashika nafasi ya nne ilhali Ureno wakishika nafasi ya tano Colombia na England wakishika nafasi ya sita na ya saba, Italia nafasi ya nane Uholanz nafasi ya tisa na nafasi ya kumi ikishikiliwa na Equador.
Katika orodha hiyo ya Viwango Afrika Kusini imefanikiwa kupanda kwa nafasi sita juu na kuingia katika kumi bora ya Afrika.
Bafana Bafana sasa iko katika nafasi tisa barani Afrika na kushika nafasi ya 56 duniani.
Mabingwa wa African Nigeria dabo wako katika yao ya nne na kushika nafasi 28 duniani na licha ya mafanikio yao ya hivi karibuni hawajaweza kupanda kutoka nafasi ya nne barani Afrika.
Equatorial Guinea , washindi wa pili Afrika wametereza mpaka nafasi ya 10 Africa, huku Cameroon wakitoka kabisa katika nafasi kumi bora.
Senegal wameingia katika nafasi ya 20 za juu barani Afrika baada ya kupanda kwa nafasi 12 na kuwaweka katika nafasi ya 76 duniani.
Top 10 in Africa:
1. Ivory Coast (12th in the world)
2. Ghana (22)
3. Mali (26)
4. Nigeria (28)
5. Algeria (35)
6. Tunisia (41)
7. Zambia (46)
8. Burkina Faso (50)
9. South Africa (56)
10. Equatorial Guinea (61)
No comments:
Post a Comment