Wachezaji wa Yanga na mashabiki wakiwa na kombe |
Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea |
Mwamuzi Martin Saanya akipatiwa huduma ya kwanza |
Mshambuliaji wa Simba akiwa amebebwa na mashabiki wa Yanga ambao waliondoka naye |
Shabiki wa Yanga akishangilia kwa staili ya aina yake |
Shabiki wa Yanga akipelekwa kupewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia wakati mchezo ukiendelea.
Beki wa Yanga David Luhende akiondosha mpira kwenye himaya ya mshambuliaji wa Simba Amri Kiemba |
Yanga ya Dar es Salaam leo
imetwaa taji la 24 la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bara ya
kuifunga Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa kufunga pazia la Ligi uliochezwa
uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Yanga
inamaliza msimu wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 60, ikifuatiwa na Azam FC yenye 52
na Simba 45
Mchezo huo ulianza kwa kasi
ambapo Yanga walifanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Didier
Kavumbangu dakika ya tano kwa kichwa ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Simba ilipata nafasi ya
kusawazisha dakika ya 27 baada ya Mrisho Ngassa kuangushwa kwenye eneo la hatari
na Nadir Haroub na ndipo mwamuzi Martin Saanya kuamuru penalti, lakini mkwaju
wa Mussa Mudde dhaifu ulipanguliwa na Ally Mustafa ‘Barthez’ kabla ya kipa huyo
kuuchupia na kuudaka.
Kipindi cha pili, Simba SC
walikianza vizuri dakika 10 za mwanzo wakipeleka mashambulizi langoni mwa Yanga
kutokea pembeni, lakini safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Bara ilisimama imara
kukabiliana na hatari zote.
Dakika ya 62 Hamis Kiiza
aliunganisha krosi maridadi ya Simon Msuva na kuipatia Yanga bao la pili. Baada
ya bao hilo, Yanga walianza kucheza kwa kujiamini zaidi na Simba wakionekana
kucheza ili kutoruhusu mabao zaidi.
Mwamuzi Saanya dakika 87
aligongana na mchezaji na kuchanika kichwani wakati anakwenda kuamua ugomvi kati ya Didier
Kavumbangu na Nassor Masoud ‘Chollo’ akaanguka na kutibiwa kwa dakika hadi
kuinuka dakika ya 90 na kumaliza mpira baada ya sekunde kadhaa.
Mchezo huo uliochezeshwa na Martin
Saanya wa Morogoro, akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jesse Erasmo
kutoka Morogoro, na mezani alikuwepo Hasim Abdallah wa Dar es Salaam.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor
Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Mussa Mudde, Shomary Kapombe, William Lucian
‘Gallas’, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme/Ramadhani Singano
‘Messi’, Amri Kiemba/Jonas Mkude na Haruna Chanongo/Felix Sunzu.
Yanga SC, Ally Mustafa
‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Frank
Domayo, Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza/Niaar Khalfan.
No comments:
Post a Comment