KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 11, 2013

HATMA YA MARTIN SKRTEL LIVERPOOL KUJULIKANA WIKI IJAYO LAKINI WENYEWE WANASAKA MLINZI WA KUCHUKUA NAFASI YAKE. HUENDA AKAELEKEA NAPOLI.

Out of favour: Skrtel lost his place in Liverpool's defence for Jamie Carragher
Add Skrtel alipoteza nafasi yake mbele ya Jamie Carragher.
 HATMA ya mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel huenda ikajulikana wiki ijayo wakati ambapo wakala wake wakitarajia kusafiri kwa ajili ya mazungumzo.
Tetesi zaidi juu ya hatma ya mlinzi huyo kisiki wa kimataifa wa Slovakia zimezidi kuzagaa kufuatia kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza mbele ya mstaafu Jamie Carragher.
Amekuwa akihusishwa na kutaka kuelekea kwa Rafael Benitez baada ya kuajiriwa na klabu ya Napoli coach.
Relaxed: Martin Skrtel and his wife Barbora were pictured while on holiday in Miami earlier this week
Martin Skrtel akiwa na mkewe Barbora katika mapumziko huko Miami
 
Licha ya wakala wake Karol Csonto kusema kuwa klabu hiyo ya Italia itatakiwa kuongea na Liverpool kwanza, hata hivyo ameshindwa kukanusha taarifa za mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 kuwa sasa anaelekea katika ligi kuu ya soka ya nchini Italia Serie A.
Amenukuliwa wakala huyo na redio moja inayoitwa Radio Crc akisema 
'Bado hakuna mawasiliano baina ya klabu hizo mbili. Martin ana mkataba na Liverpool na ni vizuri ukaheshimiwa"

'Ni wazi Napoli wanamjua Martin vizuri , lakini hakuna mawasiliano baina yetu na watatakiwa kufanya kwanza mawasiliano na kufikia makubaliano na Liverpool.

'Kuna mahusino makubwa baina ya Martin Skrtel na Rafa Benitez ambayo yamekuwepo kwa miaka mingi waliyokuwa pamoja Liverpool.
'Kiungo wa Napoli Marek Hamsik na Skrtel ni marafiki wazuri na walikutana wiki iliyopita.

Liverpool kwasasa wanamfukuzia mlinzi wa kati wa Schalke Kyriakos Papadopoulos kuchukua nafasi ya Carragher lakini pia wameonyesha nia ya kutaka wengine kwa kuziba pengo la Skrtel na huenda kukafanyika mabadiliko makubwa sehemu ya Ulinzi.
In the balance: Skrtel could leave Liverpool for Serie A side Napoli
 
Liverpool inakaribia kumchukua mshambuliaji wa Celta Vigo Iago Aspas, ambaye kwasasa anafanyiwa vipimo vya afya ndani ya Merseyside.
Mpango huo unagharama ya pauni milioni £7.7 na umekuwa katika mchakato kwa wiki kadhaa na hatimaye mafanikio yanafikiwa baada ya ligi ya Hispania kufikia ukingoni.

No comments:

Post a Comment