Lionel Messi amewasili barani Afrika katika nchi ya Senegal hii leo kwa ndege maalumu na kupata mapokezi makubwa katika uwanja wa ndege wa Dakar kutoka mashabiki wa soka wakiwemo watoto ambao wametoka sehemu mbalimbali barani humu.
Nyota huyo wa Barcelona amealikwa na akademi ya Qatar’s Aspire Football,
ambayo ina tawi nchi humo kwa ajili ya kuhudhuria katika kampeni ya kupambana na malaria.
Vyandarua kwa maelefu ambayo vina sura ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina vitagawiwa kwa watoto na familia mbalimbali kutoka maeneo ya vijijini hii ni kwa mujibu wa waandaaji.
Messi atasafiri kwa helkopta kuelekea Saly, karibu na mji mkuu wa Dakar, ambako atatembelea nyumba ya kulelea watoto na kufanya mazungumzo na wanyeji juu ya kujizuia na malaria.
Mamadou Ba ni daktari mjini Dakar amesema.
“Tunafuraha kumkaribisha Lionel Messi, na anatembelea wakati ambapo Rais wa Marekani Barack Obama akiwa nchini, tumefarijika sana ,”
No comments:
Post a Comment