Mwanariadha mashuhuri wa
Ethiopia Haile Gebrselassie ametangaza kujiunga na siasa kwa matumaini
ya kushinda ubunge hapo mwaka wa 2015.
Tangazo hili linajiri kukiwa na duru kwamba
nyota huyo wa Olimpiki anapanga kustaafu kutoka riadha. Haile ni mshindi
mara mbili wa mbio za 10,000 katika michezo ya Olimpiki na anashabikiwa
na wengi nchini Ethiopia. Hata hivyo hajatangaza chama cha kisiasa
ambacho atatumia kuwania ubunge.
Kwa miaka mingi bunge la Ethiopia limethibitiwa
na wabunge wa chama tawala cha People's Revolutionary Democratic Front
(EPRDF). Kuna mbunge mmoja pekee wa upinzani.
Akijibu mashabiki wake kupitia Twitter, Haile
alisema ni kweli kwamba ananuia kujiunga na siasa mwaka wa 2015.
Alitanagaza kustaafu mwaka wa 2010 lakini akarejea tena uwanjani na
mwezi Aprili alishinda mbio za nyika za Vienna.
Pia alishiriki Marathon ya Boston iliyokumbwa na shambulio la bomu ambapo watu watatu walikufa na makumi kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment