KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 30, 2013

Micho amfananisha muuaji wa magoli mawili dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Nambole kuwa ni kama Didier Drogba.

 


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes'  Milutin 'Micho' Sedrojevic amelinganisha ubora wa magoli anayofunga mshambuliaji wake Frank Kalanda na magoli anayofunga mfungaji wa wakati wote wa Ivory Coast Didier Yves Tebily Drogba.

 Drogba ambaye kwasasa anaichezea klabu ya Galatastaray ya Uturuki ndio mshambuliaji anayedhaniwa kuwa ni mfungaji mwenye magoli ya kusisimua barani Afrika na Ulaya wakati akivichezea vilabu mbalimbali kuanzia wakati huo katika vilabu vya Le Mans, Guingamp, Olympique De Marseille vya nchini Ufaransa na vilabu vingine vya England na Uchina vya Chelsea na Shanghai Shenhua.

Akimzungumzia mshambuliaji huyo Micho amenukuliwa akisema 
"Anapolitafuta goli, njaa yake ya kutaka kutikisa nyavu, nguvu, uwezo wa kulinda mpira na ari kubwa ya Kalanda anafanana kabisa na style ya uchezaji wa Didier Drogba".

Wakati hayo yakiwa hivyo kocha huyo mzaliwa wa Serbian ameweka wazi kuwa Kalanda bado ana safari ndefu ya kuthibtisha ubora wake na kipaji chake.

"Ni zao la kipindi cha kati, anahitaji kumalizia kujiimarisha zaidi kwa kupiga polishi kipaji na kuwa nyota wa dunia. Kitu kizuri ni kijana na ana kiu ya kujifunza "

Micho amemfananisha pia na mshambuliaji wa zamani wa Sports Club Villa , Ekuchu Kasongo, ambaye alikuwa anacheza kwa style ya Kalanda's. "

Frank Kalanda mshambuliaji kijana mwenye umri wa miaka 21, alifunga gopli safi katika mchezo dhidi ya Tanzania katika mchezo wa pili wa marudiano wa michuano ya wachezaji wa ligi za ndani barani Afrika CHAN mchezo uliopigwa katika uwanja wa Namboole maarufu kama uwanja wa Mandela mwishoni mwa juma lililopita. Magoli yake mawili yaliisaidia sana Uganda kukata tiketi ya kucheza fainali ya CHAN mwakani nchini Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment